Na Elizabeth Joseph,Arusha.


Wafugaji wa Punda wametakiwa kuhakikisha wanawapeleka kliniki Punda wao wanaowafuga ili kupata chanjo mbalimbali zinatotolewa kwa Wanyama wengine kama Mbwa na Paka.

Kauli hiyo imetolewa na Frank Pangani ambaye Daktari wa Mifugo kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Arusha linalojishughulisha na Ustawi wa Wanyama(ASPA).

Amesema kuwa wafugaji wengi wenye mnyama Punda wamekuwa wakikumbuka kuwahudumia kama Ng'ombe na Mbuzi kwa kuwapa chanjo za Magonjwa mbalimbali huku wakiwasahau Punda kuwa nao wanastahili chanjo na matibabu hasa katika vidonda wanavyopata.

"Punda anatakiwa apewe chanjo ya Pepopunda,usafi wa matibabu ya vidonda pamoja na ukaguzi na ushauri wa matibabu ya Magonjwa mengine yanayowashambulia lakini baadhi ya wafugaji wanawasahau Punda wao katika hayo jambo linaloweza kusababisha vifo kwa Wanyama hawa"alifafanua Dokta.

Ameongeza kwa kutaja adhabu mtu anayoweza kupewa kutokana kumsababishia Punda jeraha kuwa ni pamoja na kifungo cha jela mwezi mmoja ama kulipa faini isiyozidi shilingi 100,000.

"Yapo makosa na adhabu za kutesa wanyama na sheria inasema Mtu akibainika kumpiga mnyama yeyote akapata jeraha faini isiyozidi 100,000 au jela mwezi mmoja ama vyote kwa pamoja hivyo wafugaji wa Punda wanatakiwa kuijua hii na kuifanyia kazi ili kuepuka hii adhabu maana katika kliniki zetu tunazofanya kwenye minada Punda wengi tunawakuta na vidonda ambavyo vingi vimetokana na mizigo wanayobeba"ameongeza Dokta Pangani.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: