Na Lucas Myovela_ Arusha.

Hayo yameelezwa na Mawaziri wa viwanda na Biashara wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamuhuri ya Kenya walipotembelea mpaka wa Namanga ili kujione namna ya shughuli zinazo fanya mpakani hapo ili kuweza kuondoa changamoto kwa wafanya biashara wa Nchi hizo.
Akizungumza na watumishi wa mpaka wa Namanga Waziri wa Viwanda na Biashara Nchi Tanzania Prof Kitila Mkumbo, ameeleza kuwa kuliwa na changamoto nyingi za kibiashara lakini mpaka sasa wameyamaliza na mengine yaliyo baki wataendelea kuyafanyia kazi ndani ya miezi mitatu.

"Leo hii kwa ujumla wetu tumeweza kuja hapa mpakani kuona namna ya utendaji wa kazi unavyo endelea kwa mashirikiano mazuri na kiukweli tumefurahishwa na umoja wenu mlio nao hapa mpakani kama watumishi na haya yanakuja baada ya viongozi wote wakuu kuliona hilo na sisi kama watendaji lazima tuyafanikishe hayo ili kuona Nchi zetu zinapiga hatua". Amesema Prof Mkumbo.
"Katika utendaji wenu wa kazi nendeni msimamie vyema maadili ya kazi kwa wananchi haswa katika utatuzi wa vikwazo kwa wafanya biashara ili kuondoa sitofamu kwa viongozi wetu wakuu. Tunataka furaha kati ya watanzia na wakenya na uchumi wetu ukue kwa manufaaa ya nchi zetu hizi mbili na wanachi wake kunufaika kiuchumi niwaimbe sana nyie kama watumishi kuzingatia haya na pale mnaposhindwa hakikisheni mnawasiliana na viongozi husika". Prof Kitila Mkumbo.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Nchini Kenya Mhe, Betty Maina, ameeleza kuwa Tanzania na Kenya wamekubaliana kwa pamoja kumaliza changamoto zilizo kuwepo ili kutoa fursa kwa wafanyabiasha wa Nchi zote mbili kufanya kazi kwa uhuru kwa manufaa ya mataifa yao katika nyanja za kiuchumi.


"Watu wanao husika na biashara tunawaomba sana kutii sheria maana mmekuwa ni watu wa kutokutii sheria, Sasa ni muda wa kuzingatia sheria haya ni maagizo na sio maombi na kama kutakuwa na changamoto ni vizuri mkafanya mawasiliano na viongozi wenu". Ameeleza Waziri Maina.
"Na kama utashindwa kufanya biashara kwa kufuata sheria ni bora kujipanga maana Kenya na Tanzinia ni mataifa yenye uchumi mkubwa na hatupo tayari kuangusha uchumi uliyo tengenezwa na wanachi wetu. Hii vita yetu tumegundua imewapatia nafasi mataifa mengine kuleta bidhaa zao katika mataifa yetu wakati sisi bidhaa hizo tunazo na tunaweza kufanya biashara kwa pamoja ndiyo maana tumeondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi zetu". Waziri Maina.
Kwa upande wao Mabalozi wanao  ziwakilisha Nchi hizo Mbili yani Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamuhuri ya Kenya, wameeleza kuwa kwa malidhiano yaliyo fanywa baina ya mataifa haya mawili ni dhahili uchumi utaenda kukua vyema na wao kama wawakilishi watahakikisha wafanya biashara wa nchi hizo wanawekeza kwa wingi kwa manufaa mapana ya kiuchumi.
Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Dan Kazungu, ameele kuwa yeye kama mwakilishi wa Rais amefurahishwa na uamuzi wa mawaziri wa pande zote mbili kufanyia kazi maagizo ya Marais ambao walitoa muda wa mwezi mmoja kuondoa vikwazo vya kibiasha na mawaziri hao kufanya jambo hilo kwa wakati.

"Furaha yangu ni kuona tunafanya kwa pamoja maana tunapo tofautiana tunatoa mianya kwa wafanya biashara wa mataifa mengine kuingia ndani na kuchua nafasi hizo za biashara kwasasa hatuto nunua bidhaa kutoka masoko ya nje ili kudhibiti soko letu kwanza".
Amesema Balozi Kazungu.

"Pia kwa ushirikiano huu uongeza wigo katila soko la jumuiya ya Africa Mashariki na kudhibiti m'badala soko lote la Africa pia na masoko mengine kama Asia,Bara la Ulaya na Marekani, Nchi hizi mbili zinaweza hasa zikishikana vizuri tunaweza kufanya mengi zaidi na tutakuwa tumeleta utajiri nyumbani". Aliongeza Balozi Kazungu.
Nae Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt John Stephen Simbachawene, ameeleza kuwa mafanikiao haya ni kufuatia ziara ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan Nchini kenya na kutaka wataalam kutatua kero za wafanya biashara wa pande zote mbili.

"Kwa upande wangu kama Balozi nimefurahishwa sana na kikao hiki kilicho fikia maadhimia ya kuondoa vikwazo kwa wafanyabishara na Mimi kama Balozi nitahakikisha tunaendeleza mahusiano mazuri zaidi kati ya Kenya na Tanzania na wafanya biashara wa pande zote waweze kufanya biashara pasipo kuwa na vikwazo". Ameelza Balozi Simbachawene.

"Nitahakikisha pia nitaboresha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Kenya pia nitaweza kuwashawishi watanzania kuweza Nchini Kenya na Wakenya kuwekeza Nchini Tanzania kwa maslahi mapana ya uchumi ya Nchi zetu zote mbili". Ameongeza Balozi Simbachawene.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: