Na mwandishi wetu,Mbeya


MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa Uchumi na fedha Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji ,Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa mchango wa shilingi milioni 1.moja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana Mbeya Mjini.


Mahundi amekabidhi mchango huo jana ili kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana inayojengwa eneo la Isyesye Jijini Mbeya.


"Nichukue fursa hii kumpongeza Dkt Tulia Ackson kwa kutoa mifuko mia moja ya saruji ili kuendeleza ujenzi",alisema Mahundi.


Aidha amewashukuru wadau wengine wanaoendelea kuchangia ujenzi lengo nyumba ikamilike mapema ili Katibu aweze kuhamia.


Akipokea mchango huo Katibu wa Vijana Wilaya ya Mbeya Mjini Stephen Shija amemshukuru Mbunge wa Viti Maalum Mhandisi Maryprisca Mahundi kwani pesa hizo zitasaidia kulipa mafundi na kununua vifaa vya ujenzi.


Shija ametumia nafasi hiyo pia kuwashukuru wadau wengine akiwemo Ndele Mwaselela aliyejitolea mabati pia Mstahiki Meya Jiji la Mbeya Dour Issah Mohammed aliyejitolea gharama za kutandaza nyaya za umeme nyumba nzima.


Mchango wa Mhandisi Maryprisca Mahundi utachochea kasi ya kumalizika nyumba hiyo.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: