Ridhiwani Kikwete,  mtoto wa rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema baba yake ni mzima wa afya.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 27, 2021 kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram,  akijibu madai yaliyoanza kusambaa mitandaoni tangu jana kuhusu kiongozi huyo mstaafu.

Katika ujumbe wake huo,  Ridhiwani amesema, "baada ya kupokea simu na jumbe mbalimbali nimeona nitumie nafasi hii kuweka kumbukizi sawa. Mzee wetu na Mzazi wetu Dk Kikwete yupo salama wa afya nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za kipuuzi na za kupuuzwa.”
Share To:

Post A Comment: