MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Mhe Yustina Rahhi amefanya ziara Mkoa wa Manyara na kuzungumza na Baraza la Jumuiya ya Wanawake UWT Wilaya zote na angenda zake mbalimbali.


Katika ziara zake mhe Rahhi amejadili changamoto mbalimbali za kina mama na namna ya kwenda kuzitatua.

Moja ya changamoto kubwa aliyokutana nayo ni uhaba wa maji na amesema kuwa maeneo mengi ya Mkoa wa Manyara yana uhaba wa maji hivyo yeye kama mwakilishi wa kina mama amelichukua tatizo hilo na kulipeleka Bungeni tayari kwa kwenda kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Vilevile Mbunge huyo amewaasa kina mama kusimamia elimu ya mtoto wa kike na amesema ili mtoto wa kike aweze kutimiza ndoto zake ni lazima asimamiwe vizuri katika kupata elimu na hilo ni jukumu kubwa la kina mama na amesema ukimpa mwanamke elimu vizuri anakuja kuwa kiongozi bora, mchapakazi na mwadilifu.

Changamoto nyingine ya wanawake ni unyanyaswaji ambapo mhe Rahhi amekemea tabia ya baadhi ya wanaume kunyanyasa wanawake zao.
Na hilo Mbunge huyo amelichukua na kwenda kulisemea zaidi Bungeni ili kuona namna bora zaidi ya kuweza kusimamiwa vizuri katika maeneo yote ndani ya Mkoa wa Manyara.

Mhe Mbunge pia amegusia suala la Afya na hili ameliasa kwenda kupigania kuongezwa kwa madawa katika hospital za Mkoa wa Manyara, pia ili kina mama waepukane na changamoto za huduma za kliniki ni lazima uboreshwaji wa huduma upatikane.

Pia amesema ili wakina mama waweze kujidhatiti kwenye ujasiriamali vizuri ni lazima huduma muhimu kama maji, elimu na afya wawe wamezipata vizuri huduma hizo.

Hata hivyo, Mbunge huyo amewaasa wanawake kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ya kuiongoza nchi pendwa Ya Tanzania.
Mbunge huyo alianzia ziara yake Wilayani Mbulu mwezi wa nne 2021  na Mei 7 mwaka huu akaelekea Wilaya za Simanjiro, Kiteto, Hanang’ na Siku ya Mei 10 akamalizia Wilaya za Babati Mjini na Babati Vijijini katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Manyara.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: