Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo ameshiriki na viongozi wa Kata ya Chigongwe kukagua zoezi la kufungua barabara yenye urefu wa kilomita 5.2 kutoka eneo la Chigongwe-Ngh’ambala ikiwa ni sehemu wa utekelezaji wa Ahadi za Mbunge huyo za kufungua barabara hiyo ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi wa eneo hilo.


Kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza adha ya matumizi ya muda mrefu ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ndani ya kata ambapo awali wananchi walikuwa wakipata tabu kupita maeneo yasiyo rasmi kwasababu ya kukosekana kwa barabara inayounganisha mitaa husika.


“Tumeanza sasa ukarabati na kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali za ndani ya Jiji na pembezoni ya Jiji ili kuwapunguzia adha wananchi kutokana na kutopitika kwa urahisi kwa baadhi ya barabara katika maeneo mbalimbali.


Nitendelea kushirikiana na TARURA kuhakikisha tunayafikia maeneo mengi zaidi yenye barabara korofi kadri bajeti itakavyoruhusu”Alisema Mavunde


Naye  Diwani wa Kata ya Chigongwe *Mh. Simon Machela* amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutekeleza ahadi hiyo ya ufunguzi wa barabara ambayo itasaidia kuchochea shughuli za maendeleo katika eneo hilo na pia itarahisisha usafiri kwa wananchi hao kutoka eneo moja kwenda nyingine bila usumbufu tofauti na ilivyokuwa awali.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: