HOSPITALI ya Miracolo inatarajia kupima  afya bure kwa wakazi Jimbo la Segerea  Jijini Ilala siku ya Jumamosi Mei 29 mwaka huu. 

Matibabu hayo ya afya bure kwa magonjwa mbalimbali yanatarajia kuanza saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni  kituo cha dalaadala Segerea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa shughuli hiyo daktari Bingwa wa Watoto wa hospitali ya Maracolo, Dkt. Anna Deogratias alisema mwaka 2021 hospitali hiyo inadhimisha miaka mitano ya kutoa huduma kwa wananchi  katika madhimisho hayo wametenga siku hiyo kwa ajili ya kutoa matibabu bure kwa wakazi wa jimbo la Segerea na maeneo ya jirani .

Dkt. Anna alisema baadhi ya magonjwa ambayo yatapimwa siku hiyo  presha, Kisukari,Wingi wa damu, Virusi vya UKIMWI,afya kinywa na meno na magonjwa nyemelezi .

Aidha Dkt, Anna alisema pia watakuwepo wataalam Bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa ushauri wa afya kwa wananchi watakaojitokeza kupewa matibabu .

Alisema kujua afya yako mapema ni muhimu wananchi wengi wamekuwa wakishindwa kuangalia afya zao kwa wakati hospitali ya Maracolo inaunga mkono juhudi za serikali katika kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na  ndani ya miaka mitano Hospitali ya MIRACOLO imepata mafanikio makubwa pia wameshirikiana na Serikali vizuri katika suala zima la afya.

Share To:

Post A Comment: