Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya mashtaka imewafikisha mahakamani watumishi 6 kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha James Ruge alisema watuhumiwa ambao ni wakazi wa tarafa ya Eyasi iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Karatu ambapo ni wafanyakazi wa mradi wa LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM unaohusika na ukusanyaji wa ushuru wa utalii wa kitamaduni katika kata ya Mang'ola.
Ruge alisema kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la kuisababishia halmashauri ya wilaya ya Karatu hasara ya shilingi milioni kumi na moja Laki nne, ekfu tisa na Arobaini na tano(11409045)katika kipindi cha mwezi julai 2017 hadi mwezi machi 2018.
Aliongeza kuwa katika kipindi tajwa watuhumiwa watatu walihusika kukusanya ushuru huo ambao hawakuuwakilisha katika mamlaka husika ambayo ni halmashauri ya wilaya ya Karatu kama miongozo inavyowataka.
Aidha alisema watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Karatu mnamo tarehe 20 mwezi 4 mwaka huu kwa makosa ya uhujumu uchumi kinyume na sheria,kifungu cha 28(2) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa pamoja na kosa la kuisababishia serikali hasara kinyume na Aya ya 10(1) na vifungu vya 57(1) na 62(2) vya sheria ya uhujumu uchumi makosa ambayo yalipelekea halmashauri hiyo kupata hasara.
Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Arusha imewafikisha katika mahakamani ya hakimu Mfaeidhi wa Wilaya ya Longido watuhumiwa 3 ambao ni Cleophas Anton,Josephine Innocent na Rose Lorivi waliokuwa ni watumishi wa halmashauri ya wilaya ya longido katika kitengo cha manunuzi kwa kosa la kutumia nyaraka za uongo kinyume na kifungu cha 342 cha sheria ya kanuni za adhabu na kufunguliwa shauri ya jinai.
Aliongeza kuwa watuhumiwa hao walipaswa kufanya manunuzi ya mifuko ya saruji 2400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Engarenaitor huku mifuko ya saruji 180 haikuwasilishwa ambapo katika shauri lingine mtuhumiwa Rose Lorivi Kipuyo aliyekuwa afisa mtendaji wa kijiji cha Oltepesi katika halmashauri ya wilaya ya Longido alifikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia nyaraka za uongo kinyume na kifungu cha 342 cha sheria ya kanuni za adhabu na kufunguliwa shauri la jinai namba 51/2021
Alieleza kuwa mtuhumiwa huyo aliandika barua kuwa serikali ya kijiji hicho iligawa viwanja kwa wananchi taarifa ambayo haikuwa sahihi.
Sambamba na hayo TAKUKURU Mkoa wa Arusha ilishinda shauri namba 193/2020 lililokuwa likiendelea katika mahakama ya wilaya ya Arusha dhidi ya Elias Samwel Mollel aliyekuwa akituhumiwa kwa kumuonga askari ili ampatie dhama ndugu yake aliyekiwa akishikiliwa katika kituo cha polisi ambapo amehukumiwa kulipa faini ya shilingi 500,000 au kwenda jela kwa miaka 3.
Pia TAKUKURU mkoa wa Arusha imefanikiwa shilingi Millioni 10 na laki tatu na elfu 80 zilizokuwa zimechepushwa na kufanyiwa ubadhilifu kinyume na sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007, fedha ambazo zilikuwa ni stahiki za waliokuwa wafanyakazi wa Word Vision mkoa wa Arusha.
Post A Comment: