Na. Angela Msimbira TAMISEMI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu  amewaagiza watendaji wa  Halmashauri zote nchini  kuhakikisha wanajenga mahusiano mazuri na baraza la madiwani  ili kuweza kutimiza malengo ya serikali ya kufikisha huduma bora kwa wananchi.


Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo wakati akiongea na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Jijini Dodoma mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa  na Halmashauri hiyo 


Amewataka wataalam kuhakikisha wanazingatia  ushauri  wa baraza la madiwani  kwa kuchuja masuala ya muhimu  na yanayoonekana yanaenda kinyume na sheria na taratibu  wawashirikishe  Wakuu wa Mikoa.


“Msiwadharau Madiwani na kudhani hawajasoma, wapo madiwani wanaelimu ya kutosha,hao ndio wawakilishi wa wananchi na wamechaguliwa  na wananchi wapeni ushirikiano ili kuleta maendeleo katika Halmashauri zetu “amesema  Waziri Ummy


Amefafanua kuwa madiwani ndio wawakilishi wa wananchi na wamechaguliwa kwa ajili ya kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili , hivyo ni vyema watendaji wa Halmashauri wakahakikisha wanaimarisha mahusiano katika utendaji kazi na baraza la madiwani  ili kuleta mabadiliko na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Halmashauri.


Wakati huohuo Waziri Ummy amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya chamwino Athumani Masasi kujenga mahusiano mazuri na watumishi wa Halmashauri hiyo ili kuhakikisha wanaweka mikakati ya ukusanyaji wa mapato kutokana na halmashauri hiyo kutokufanya vizuri katika ukusanyaji wa Mapato.


Aidha amemuagiza Mweka hazina wa Halmashauri hiyokuhakikisha anapeleka benki kiasi cha shilingi milioni 139 hadi kufikia tarehe 15/04/20201 fedha ambazo zilikusanywa lakini hazikuwekwa benki

Share To:

msumbanews

Post A Comment: