MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akifungua warsha ya pili ya wadau wa Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa inayofanyika kwa wiku tatu mkoani Tanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac
Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac akizungumza wakati wa warsha hiyo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  akiwa ameshikilia kitabu chenye  Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa mara baada ya kufunga warsha ya wadau wa mpango huo wa Taifa Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla
Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla kushoto akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kitabu chenye mpango wa wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  kulia akiteta jambo na Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla wakati wa warsha hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amefungua warsha ya pili ya wadau wa Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa inayofanyika kwa wiku tatu mkoani Tanga
 
Akizungumza wakati akifungua warsha hiyo,RC Shigella alisema Serikali kupitia Shirika la uwakala wa meli Tanzania (Tasac) imekuja na mpango wa Taifa wa kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini unaotakana na umwagikaji wa mafuta kwa lengo la kuzifanya bahari na maziwa nchini ziweze kukabiliana na umwagikaji wa mafuta kutoka nchi jirani.
 
Alisema mpango huo umekuja wakati muafaka kutokana na kuongezeka kwa shughuli nyingi kwenye bahari na hivyo kupelekea uchafuzi na hatimaye kuhatarisha matumizi ya bahari kwa watumiaji. 

Alisema mpango huo utasaidia sana hasa wakati huu ambapo kumekuwa na matumizi mengi ya baharini na hivyo kuna uwezekano kukatokea uchafuzi wa mazingira. 

"Serikali imeona ipo haja ya kuja namkakati wa mpango huu wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta baharini na kwenye maziwa tumeona shughuli za baharini zinavyozidi kuongezeka na namna ambavyo shughuli za mafuta zinavyozidi kuwa nyingi…….., alisema RC Shigela na kuongeza kuwa

Kama tunavyofahamu Tanzania ina maziwa mengi sana na Tanzania ina bahari ya hindi ina zaidi ya kiliomota zaidi ya 1000 za bahari,  ni eneo kubwa ambalo linaweza kupata uchafuzi wa baharini na uchafuzi wa baharini unaweza ukatokana na meli zinazoleta mafuta lakini pia unaweza kutokea sehemu ya nchi nyingine sababu sisi tupo majirani na upande wa Mombasa na Mozambique uchafuzi unapotokea huko upo uwezekano wa kuja upande wa kwetu wa Tanzania. 

Alisema endapo patatokea tatizo la kumwagika mafuta nchi jirani upo uwezekano mkubwa wa madhara yake kufika mpaka nchini mwetu na ndio maana serikali imeona ipo haja ya kuja na mpango utakaotumika kwajili ya kukabiliana na uchafuzi huo. 

Shigela alisema mpango huo hauhusu eneo la baharini pekee bali unahusisha mpaka maziwa ya Tanganyika,  Victoria na Nyasa kutokana na kuwepo kwa muingiliano mkubwa wa shughuli za kibinadamu katika maziwa hayo. 

Hata hivyo Shigela alisema mpango huo umekuja wakati muafaka ambapo serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya shughuli za baharini kwa kupanua meli zetu kwa kujenga misingi na gati nzuri ambazo zitatumia meli kubwa lakini pia kwa kushuhudia wakati wowote ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kuja bandari ya Tanga unaanza kutekelezwa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac,  alisema kuwa majukumu ya Tasac ni kusimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini na kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za usafiri wa majini ambapo katika jukumu hilo shirika husimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya shirika la bahari duniani (IMO)  iliyoridhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania. 

Mkurugenzi huyo alisema kutokana na majukumu ya Tasac ni kazi ya msingi ya shirika kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na umwagikaji wa mafuta kutoka kwenye vyombo vya usafiri majini kwasababu hiyo shirika kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali liliandaa mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa mwaka 2016.

Mpango huo ulifanyiwa mabadiliko mwaka 2020 na kuidhinishwa na waziri wa ujenzi na uchukuzi kama nchi walibaini umuhimu wa mpango na kuuandaa kwasababu unakidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. 


Mwisho.

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: