MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe Neema Lugangira akizungumza wakati akichangia mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wa kuboresha Mpango wa Maendeleo ya Taifa uliojikita kuishauri Serikali kupunguza gharama kubwa ya kuwalisha chakula mahabusu ili fedha zitakazookolewa zielekezwe kwenye utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.
 

MBUNGE wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs); Mhe Neema Lugangira ameibua mjadala mpya kuhusu mamilioni ya fedha ambazo zimekuwa zikitumika kila mwezi kulisha chakula mahabusu hapa nchini baada ya kuishauri Serikali ichukue maamuzi madhubuti ya kuona namna ya kupunguza idadi ya mahabusu waliopo magerezani ili kupunguza gharama hizo zinazotumika.

Mbunge Neema ameibua mjadala huo wakati akichangia mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wa kuboresha Mpango wa Maendeleo ya Taifa uliojikita kuishauri Serikali kupunguza gharama kubwa ya kuwalisha chakula mahabusu ili fedha zitakazookolewa zielekezwe kwenye utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.

Alisema iwapo idadi hiyo ikipunguzwa itasaidia kuokoa fedha ambazo hivi sasa Jeshi la Magereza linatumia Milioni 900 kila mwezi  kwa aili ya chakula cha Wafungwa na Mahabusu zitasaidia katika masuala mengine mbalimbali ya kimaendeleo hapa nchini.

Mbunge Neema alisema alisema anaamini kwamba wanapozungumzia kuchangia kuboresha Mpango wa Maendeleo ya Taifa ni lazima pia waangalia namna ya kupunguza mzigo usiokuwa na lazima kwa Serikali na ili Fedha zitakazookolewa ziekelezwe eneo jingine ambalo linastahili kwa sababu yeye binafsi anaona huo ni upotevu wa Fedha ambazo sio za lazima.

“Pamoja na ushauri huu Mh Naibu Spika nashauri njia nyengine ambazo Serikali inaweza kufanya ni Mahakama ibebe jukumu la kugharamia Bajeti ya kulisha mahabusu waliopo gerezani kwa sababu kimsingi wapo huko kutokana na ucheleweshwaji wa ucheleweshwaji wa kesi zao kupata
hukumu” Alisema Mbunge Neema

Aidha, Mhe Neema Lugangira aliongeza kwamba hata Jeshi la Polisi pia pengine linajukumu kwenye hili kwa sababu bila kufanya hivyo ni kuendelea kulionea Jeshi la Magereza wakati Serikali imesema lijitegemee wakati halina vyanzo mapato hivyo ni matumaini yake kwamba wakati Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe Mwigulu Nchemba atakapo wasilisha muelekeo kulingana na maoni mengi yaliyotolewa atazingatia ushauri wake maana jambo hili analijua vizuri sana ukizingita alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Katiba na Sheria.

“Kwani ni lazima Serikali ifika mahali iangalie suala la idadi kubwa ya mahabusu waliopo gerezani na nasema hivyo kwa sababu hivi sasa Tanzania ina wafungwa takribani 16,836 na mahabusu 16,703 ambapo Jeshi la Magereza kila mwezi inatumia milioni 900 kwa ajili ya kuwalisha wafungwa na mahabusu hiyo ni gharama kubwa sana kwa serikali” Alisema Mbunge Neema

“Sasa tupate picha kidogo ikiwa tutaweza kupunguza idadi kubwa ya mahabusu gezerani inamaana kati ya hiyo milioni 900 kila mweziinayotumika na Jeshi la Magereza kwa ajili ya  kulisha chakula
wafungwa na mahabusu tukiweza kupunguza idadi ya hao mahabusu ina maana kuna kiasi kikubwa cha fedha kinaweza kuokolewa na kiasi hicho iila mwezi kitakwenda kufidia kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinahitajika ili kutekeleza mipango mbalimbali na ushauri uliotolewa
na wabunge” Alisema Mbunge Neema Lugangira.

Mhe Neema Lugangira alikumbushia pia Hotuba za hivi karibu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan aliliongelea suala la idadi kubwa ya mahabusu kwenye magereza hivyo ni matarajio yake jambo hili litapewa uzito unaostahili.


MWISHO

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: