Na Ahmed Mahmoud Arusha Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika mashariki wamlilia hayati magufuli na kuahidi kumuenzi kwa vitendo kwa yale yote aliyoyafanya wakati wote wa uhai wake. Akiongea mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kwa niaba ya majeshi ya nchi sita za Jumuiya ya Afrika mashariki zinazowakilishwa ndani ya jumuiya hiyo Mwenyekiti wa majeshi hayo Kanali Rafael Kiptoo alisema tumeshtushwa sana na kifo cha aliyekuwa Amiri Jeshi mkuu hayati Dkt John Magufuli. Alisema kuwa wao kama wawakilishi wa majeshi ya nchi sita wanamuona hayati Magufuli kama kielelezo cha kiongozi mzalendo mbeba maono hivyo wao wataendeleza yale yote aliyowaelekeza wakati wote wa uhai wake. "Hayati Dkt.Magufuli alikuwa shujaa na kielelezo cha kupigiwa mfano sisi kama majeshi tutamuenzi kwa vitendo katika kuwatumikia wananchi ndani ya Jumuiya yetu” Aliwataka wananchi ndani ya jumuiya ya Afirika mashariki kuwa na subra utulivu kipindi chote cha maombolezo ya shujaa wetu na mwana wa Afrika na mpigania umoja na mshikamano ndani ya Afrika mashariki. Alisema kuwa wao kama jeshi ndani ya jumuiya hiyo ambao tunawatumikia wananchi wakati wote kwenye majanga furaha na maombolezo tunaimani tutaendeleza mshikamano umoja na vipaumbele katika kuboresha jumuiya yetu kuwa eneo salama lenye amani na utulivu kama alivyokuwa anataka kuona hayati Dkt.Magufuli.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: