WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kuhakikisha watumishi waliopaswa kuhamia katika makazi rasmi ya halmshauri zilizohamishwa wanafanya hivyo mara moja ili kuwa karibu na jamii wanayoihudumia.


Majaliwa ametoa maagizo hayo bungeni leo Alhamisi, Februari 4, 2021, wakati wa maswali na majibu baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’


“Rais alitoa siku 30 kwa halmashauri za vijijini ambazo zilikuwa zinakaa mjini zirudi kwenye maeneo husika, ni kweli wamehamisha ofisi lakini wanaenda kulala mjini, je nini kauli ya serikali kwa halmashauri hizo ambazo watumishi wanarudishwa kulala mjini?” ameuliza Msukuma.


Majaliwa amejibu: “Ni kweli rais alitoa agizo na halmashauri nyingi zililitekeleza, nataka niagize halmshauri zilizotakiwa kuhama waondoke mara moja na wasipofanya hivyo RC wa mkoa husika achukue hatua dhidi ya watu hao ambao hawataki kwenda kwenye maeneo mapya.

Share To:

Post A Comment: