Na Teddy Kilanga 


Wakuu wa shule za misingi wametakiwa kushirikiana na jamii pamoja na wazazi katika kusimamia miundombinu ya shule na wanafunzi kama wadhibiti ubora wa ndani ili kuinua kiwango cha elimu cha mtoto wa Kitanzania.


Akizungumza na wakuu wa shule za misingi wa mkoani Manyara katika mafunzo yaliyofanyikia wilayani Arumeru,Mkoani Arusha,Mtendaji Mkuu wakala wa maendeleo wa uongozi wa walimu(ADEM) Dr.Siston Masanja amesema kutokana na mfumo wa udhibiti ubora kubadilika ndio hali iliyopelekea wizara ya elimu kuandaa kihunzi cha udhibiti ubora ambacho kinajumuhisha wazazi,walezi pamoja na jamii kuwa ni moja wa wadhibiti ubora wa ndani.


"Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na wizara ya elimu sayansi na teknolojia wameanza na walimu wakuu wa awamu ya kwanza 8096 ikiwa awamu ya pili watakuwa 8127 ikiwa lengo letu ni kuwajengea uwezo na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata ikiwa lengo ni kusimamia udhibiti ubora wa shule ili kila hatua iweze kufuatilia vigezo bora vya usimamizi wa shule,"alisema


Dr.Masanja alisema udhibiti ubora ni pamoja na kuhakikisha viwango vya elimu vinasimamiwa vyema ikiwa namna ya ufundishaji kwa kufuata mitaala ya elimu inavyoelekeza,nakuweza kusimamia miundombinu mbalimbali ya elimu ikiwemo vifaa na madarasa kwa kuaandaa mazingira bora ya kufundishia wanafunzi ili mwanafunzi aweze  kusoma vizuri,"alisema Mtendaji Mkuu wa wakala wa maendeleo.


"Walimu wakuu kwa kushirikiana na jamii,wazazi,walezi pamoja na jamii kwa kuandaa mazingira bora ya kusomea wanafunzi kama wadhibiti ubora wa ndani itasaidia kuondoa  hali hatarishi kwa watoto wa shule na kwakuzingatia wale wenye ulemavu kupata msaada wa masomo kwa uhakika nakupata fursa kama wengine,"alisema Dr. Masanja.


Aidha Dr. Masanja alisema hapo awali udhibiti ubora ulikuwa chini ya wizara ya elimu lakini mfumo umebadilika ambapo jamii na wazazi wanatakiwa kushirikia katika udhibiti ubora wa ndani ambapo kwa kushirikishirikiana pamoja kutasaidia kuzalisha rasilimali watu iliyobora.



Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka(ADEM) Malimi Sai alisema kuwa jumla ya washiriki wa mafunzo 305 wameweza kuwezeshwa mada mbalimbali ikiwemo udhibiti ubora wa shule,ubora wa mitaala,ubora wa ufundishaji,ubora wa wanafunzi,ubora wa uongozi wa utawala,ubora wa mazingira ustawi elimu ya majanga shuleni na ushirikishwaji wa jamii na udhibiti ubora wa shule.


"Ni matarajio yangu kuwa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa udhibiti ubora wa shule yatakuwa chachu yakuwapa umahiri walimu  kwenda kusimamia vyema miundombinu ya elimu shuleni ili kuweza kunyanyua kiwango cha elimu cha mtoto wa Kitanzania,"alisema Mratibu huyo.




Mmoja wa walimu wakuu waliopewa mafunzo hayo kutoka shule ya msingi kaloleni halmshauri ya wilaya ya Kiteto,Mwl Grace Bartholomew alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika masuala uongozi na pamoja na walimu wakuu kwa kushirikiana na jamii,wazazi na walezi kwa kufanya udhibiti ubora wa ndani wa shule katika kuboresha taaluma.


"Mafunzo haya pia yanatusaidia katika nyanja za utawala bora ambapo sisi kama walimu tutaenda kushirikisha jamii kuwa sehemu ya maendeleo ya shule kwa kutambua na kuelewa kuwa wao ni wamiliki ili waweze kuhimarisha na kuendeleza shule zao na kupitia mafunzo haya yametufanya kufahamu namna ya kuandaa mpango kazi wa elimu,"alisema Mwalimu Mkuu huyo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: