Mbunge wa Mbeya mjini kwa kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa mkopo wa bajaji tano na pikipiki moja, vyote vikiwa na thamani ya Tsh: 39, 970,000/- kwa wanachama wa Bodaboda na Bajaji jijini hapo ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kama alivyoahidi katika kampeni zake.


“Tulipokuja hapa kuwaomba kura tuliwaambia sisi ni watu wa kazi na sio wa maneno maneno, kazi tulishaianza na hapa ni mwendelezo wa kile tulichokuwa tukikifanya. Haya ni maisha yetu ya kawaida tutaendelea na hapa tumeuwasha moto hakuna wa kuuzima”- Dr. Tulia Ackson


“Tunatamani kila mtu afanye shughuli ya maendeleo yenye kuleta tija katika maisha yake, mtaona hapa miongoni mwa waliopata mkopo wa bajaji hapa ni ndugu Mawazo ambaye yeye ni mlemavu wa miguu lakini licha ya ulemavu wake hakujibweteka na badala yake amekuwa akijishughulisha”- Dr. Tulia Ackson


“Mbeya mjini yale mambo ya kukaa vijiweni kupiga stori kuanzia asubuhi hadi jioni sasa zimekwisha na hazitufai, tunahitaji kuona kila mtu anajishughulisha ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kuzitatua katika maeneo yetu kwamaana kama hautakuwa na kipato ni kwamba hata changamoto ndogondogo za mtaani kwako hautaweza kuzitatua”-Dr. Tulia Ackson

Share To:

Post A Comment: