NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai ameuagiza uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA) kuongeza juhudi katika kujenga tawi la chuo hicho Dodoma kwani mafunzo wanayotoa hasa ya uongozi na utawala bora utawasaidia wabunge kujifunza.


Spika Ndugai aliyasema hayo katika mahafali ya 22 ya chuo hicho yaliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto ambapo  aliutaka uongozi wa chuo hicho kuongeza jitihada katika kujenga tawi makao ya nchi ili kuwafikia watanzania wengi wakiwemo wabunge.


“Tawi likiwepo Dodoma watanzania wengi wataweza kufaidika na mafunzo muhimu yanayotolewa na chuo hiki na hasa ya uongozi na utawala bora yatasaidia wabunge kujifunza,” Alisema Spika Ndugai.


Alieleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wabunge kama ambavyo chuo hicho  kilivyopanga kuyatoa kwa viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali.


Aidha aliwataka wahitimu kutumia elimu waliyoipata kufanya mengi mapya yenye kukuza uchumi wao binafsi, wafamilia na wa taifa kwa ujumla kwasababu elimu ni ukombozi na ni gharama kuipata.


“Serikali yetu,wazazi na walezi wameweka pesa nyingi kuhakikisha mnapata elimu hii hivyo tunamatarajio makubwa sana mtaleta mabadiliko kwenye jamii tunaomba msituangushe,” Aliwasihi wahitimu Spika Ndugai.


“Na nyiyi pia mlitoa muda wenu kuhudhuria katika madarasa, kuwasikiliza walimu na kufanya mitihani lakini pia walimu na wafanyakazi wa chuo wamefanya kazi kubwa kuwafundisha, kila mmoja juhudi zake zilizowafanya leo muwe katika mahafali haya, msiwaangushe,”Alisisitiza.


Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka alisema kuwa wamepokea kwa mikono miwili maelekezo ya Spika na watayafanyia kazi kwani tayari wameshatafuta kiwanja chenye ukubwa wa hekari tano Dodoma tayari kwa kuanza ujenzi wa tawi.


“Tumeshatengeneza mpango na tunatarajia January 2021 tutaanza kutekeleza mpango mkakati wa ujenzi wa tawi la chuo chetu Dodoma,”Alisema Profesa Sedoyeka.


Alifafanua kuwa chuo hicho kimejipanga kuboresha mitaala yake ambapo awali walikuwa na mitaala ambayo inawatengeneza wahitimu kwenda kutafuta ajira lakini hivi sasa wanatengeneza wahitimu wahitimu watakaoenda kutengeneza ajira.


Alisema wameanzisha Kituo maalum cha biashara(Kituo hatamizi)ambacho mtu ataenda na wazo lake la biashara  na watamsaidia wazo hilo kuwa biashara kamili na baadae kukuza na kuwa biashara kubwa.


“Tumetenga eneo,utaratibu maalum, fedha na wataalamu ili kuhakikisha vijana watakaoenda na mawazo yao yanahama na kuwa makampuni makubwa yanayodhaliaha na kwa kufanya hivi dhana ya uchumi wa kati itaenda vizuri,”alisema.


Aliendelea kusema kuwa ya Kituo hicho ni mtu kujiajiri na kuajiri wengine na mwisho kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuchangia katika pato la taifa.


Alisema wanaendelea kutengeneza mitaala mipya ambayo muelekeo wake ni kujifunza kwa vitendo ambapo wameshaanza katika fani ya uhasibu na utalii.


Hata hivyo katika mafali hayo wamehitimu wanafunzi 1952 katika ngazi ya astashahada,stashahada, shahada na shahada za uzamiri katika fani mbalimbali.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: