Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kitengo cha Takwimu Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Khamis Mwinyi Bakari akijibu baadhi ya Maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari katika hafla ya  Utoaji wa Takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto katika hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mayasa Mahfoudh akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusiana na shamra shamra kuelekea kilele cha siku ya Takwimu Afrika hafla iliofanyika  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ramla Hassan Pandu akitoa Takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto kwa Mwezi wa Octoba 2020 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Nasma Haji Chumu akitolea ufafanuzi juu ya maswala ya  Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto katika hafla  iliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.

Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya Utoaji wa Takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto iliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar

Na Mwashungi Tahir 

IMEELEZWA  kwamba Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa karibu na  watoto wao ili wanapofikwa na vitendo vya udhalilishaji waweze kuwaeleza baada ya kuonekana vitendo hivyo vinaongezeka Zanzibar kila siku.

Hayo ameyasema Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi Khamis Mwinyi Bakar   katika kikao na waandishi wa habari huko katika Ofisi ya Mtakwimu iliopo Mazizini wakati wa ikiwasilishwa  takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia  kwa wanawake na watoto.

Amesema wazazi wengi wanakuwa na tabia ya kupuuza taarifa za awali za udhalilishaji ambazo wanapewa na watoto wao  jambo ambalo linapelekea vitendo hivyo kuzidi kukua zaidi hadi kuwaathiri.

“Tuwe na tabia ya kuwa karibu na watoto wetu ili kuwabaini kwa haraka pale wanapofanyiwa  vitendo vya udhalilishaji  na kuvipatia ufumbuzi kwa haraka.” Alisema Khamis Bakari.

Akiwasilisha takwimu za udhalilishaji za mwezi Oktoba 2020 Mtakwimu kitengo cha Makosa ya Jinai, Madai na Jinsia Ramla Hassan Pandu amesema jumla ya matukio 103 ya ukatili udhalilishaji na jinsia yameripotiwa idadi ambayo  inaonekana kushuka ukilinganisha na mwezi wa Septemba 2020 ambapo jumla ya matokeo 116 yaliyoripotiwa.

Amesema Wilaya ya Mjini imeripotiwa kuwa na matukio mengi zaidi ikilinganishwa na Wilaya nyengine ambapo matukio 29, ikifuatiwa na Magharibi ‘B’matukio 19, Wilaya ya Kaskzini “A” na  Kusini ina idadi ndogo zaidi ya matukio kuliko zote matukio mawili kwa wilaya zote.

Aidha amesema takwimu zinazotolewa zinahusu aina za ya matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia  kwa wanawake na watoto ambayo yameainishwa katika matukio makuu sita ikiwemo kubaka,kulawiti,kuingiliwa kinyume na maumbile . kutorosha,shambulio la aibu/kukashifu na shambulio.

Nae Mkurugenzi wa wanawake na watoto kutoka Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na watoto Nasima Haji Chum amesema ni jukumu la wazazi kushirikiana katika suala la malezi il kuendelea  kupunguza vitendo vya udhalilishaji.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu  wa Serikali Mayasa Mahfoudh Mwinyi amewataka wadau wa maswala ya udhalilishaji kuhakikisha masuala ya udhalilishaji yanapungua ili kutimiza azma ya Serikali.

Mkutano huo ni endelevu ambao  kila  mwezi ripoti  za udhalilishaji hutolewa  ambapo imefuatana na miongoni mwa shamrashamra za kuelekea siku ya Takwimu za Afrika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu.

 Uboreshaji wa mifumo ya Takwimu kitaifa kwa uzalishaji wa Takwimu na utoaji wa Taarifa ili kuwepo kwa amani na Maendeleo endelevu Barani Afrika.


Share To:

msumbanews

Post A Comment:

Back To Top