Na Joseph Ngilisho,Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira,amewataka viongozi wa upinzani wanaopanga kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi uliokipa ushindi chama cha mapinduzi ccm,kutofanya hivyo badala yake wakimbilia mahakamani kudai haki wanayoitaka.


Mghwira ametoa kauli hiyo mapema Leo jijini Arusha wakati alipohudhulia siku ya  matanga ya msiba wa kaka yake ,mfanyabiashara Philemon Mollel na kueleza kuwa maandamano sio suluhisho la kudai haki ispokuwa njia pekee ya kudai haki ni kwenda mahakamani.


"Kwa ujumla Mkoa wa Kilimanjaro upo Shwari ila tumewashauri wanaojipanga kutaka kuandamana kutofanya hivyo badala yake waende mahakamani wakadai haki wanayoitaka" alisema Mghwira


Aidha aliongeza kuwa madai ya wanasiasa kuyafanya kuwa madai ya wananchi jambo hilo si sahihi sana ,chamsingi wanasiasa wapiganie haki yao kwa njia sahihi na si haki ya wananchi maana wananchi wamefanya uamuzi wao kwa kuwachagua viongozi waliokuwa wakiwahitaji.


Akiongelea hali ya usalama mkoani huo  ,amesema kuwa hali ni shwali na hapakuwepo na mtu yoyote aliyeandamana mkoani humo na kuendelea kuwataka wananchi kuwa watulivu ili wasije kujitumbukiza  kwenye vurugu zinazoweza kuhatatisha maisha yao.


Hata hivyo Mngwira alikiri kuwa upinzani bado ni mkali mkoani kilimanjaro Ila kwa kuwa washindi wamepatikana wananchi hawanabudi kuwa watulivu na kuwataka kuendelea na maisha yao ya kila siku, kwani kuna Maisha baada ya kuchaguzi.


Katika hatua nyingine Mgjwira alikiri kuwa hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa kuhusiana na matukio ya uchaguzi .

Share To:

msumbanews

Post A Comment: