NA HERI SHAABAN
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Segerea tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bonah Ladslaus alisema atakapochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea ataelekeza Maendeleo Kata ya Kimanga kwa kujenga Barabara ya Mwendo Kasi kwa ajili ya mabasi ya Haraka na vituo vya Afya.
Bonah alisema hayo leo katika kampeni Kata ya Kimanga wakati akitamburishwa kwa wananchi na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Idd Mkoa.
Bonah aliwataka wakazi wa Kata hiyo kuchagua Diwani wa CCM Pastory Kombya ili aweze kushirikiana kuleta maendeleo ya kata pamoja na Jimbo la Segerea .
"Nitakapochaguliwa Mbunge wa Jimbo ili na diwani wangu tutawajengea kituo cha afya,kituo cha daladala cha kisasa , pamoja na barabara ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka UDART "alisema Bonah.
Bonah alisema awali maendeleo ya kata hiyo yalikuwa yakielekezwa kata zingine kutokana na diwani aliyemaliza muda wake alikuwa akidaiwa kukwamisha maendeleo na fedha zikitolewa na Serikali zilikuwa zikielekezwa kata zingine huku kata ya Kimanga ikirudi nyuma kimaendeleo .
Akizungumzia mikakati yake katika kata ya Kimanga alisema atasimamia yote yaliopo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi 2025 ikiwemo kuboresha miundombinu pamoja na sekta ya maji.
Mikakati mingine atasimamia vikundi vya jimbo la Segerea kuwawezesha mikopo ili waweze kujishughulisha katika uzalishaji kiuchumi.
Aliwataka Tabata Kimanga kumpigia kura mgombea Urais wa CCM John Magufuli ,Mgombea wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli na diwani wa Kimanga Pastory Kombya .
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Idd Mkoa , amewataka wakazi wa Wilaya ya Ilala kupigia kura chama cha Mapinduzi kwa Maendeleo ya Wilaya ya Ilala.
Katibu wa CCM Idd Mkoa alisema CCM imejipanga vizuri katika kushinda majimbo yake matatu yote ambapo familia ya CCM ni familia kubwa ina historia nzuri katika utendaji wake wa kazi .
Mwisho
Post A Comment: