Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemsamehe Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na kumfutia adhabu ya miezi 18 aliyokuwa akiitumikia.

Tangazo hilo limetolewa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais John Magufuli wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kinachoendelea jijini Dodoma baada ya kuomba ridhaa ya wajumbe wa kikao hicho ambao nao wameridhia Kinana asamehewe.

Rais Magufuli amesema Mzee Kinana ameonekana kujutia makosa aliyokuwa ameyatenda na kuomba msamaha, hivyo ni vema akasamehewa ili aungane na wanachama wenzake katika kukijenga chama.

Tayari Mzee Kinana ametumikia adhabu hiyo kwa muda wa miezi minne.
Share To:

Post A Comment: