Msanii wa WCB, Zuchu amewavunjia ukimya wanaomponda kutokana na aina ya muziki anaoufanya.

Zuchu amesema kuwa kuna muda anahisi hapendwi kutokana na watu jinsi wanavyomponda, lakini anapata matumaini na kujipa moyo anapoona watu wakiimba nyimbo zake.

"Wananisema mimi muimba taarabu ,na kuniponda kila kukicha kwa jinsi ya utofauti wangu wa uandishi na aina ya muziki nnaoufanya, kuna muda natetereka nahisi pengine sitopendwa,'

"Ila ona watu wakubwa wanaimba nyimbo zangu tena neno baada ya neno wamekariri mpaka melodies,"

"Mi najua huyu ni Mwenyezi Mungu ananionyesha kwamba pengine nnachokifanya sio kibaya sana napata moyo wa kuendelea" alisema Zuchu.

Ametoa maneno hayo baada ya mwanadada Elizabeth Michael  "Lulu" kupost kipande cha video akiimba wimbo wake unaoitwa Raha.
Share To:

Post A Comment: