MENEJA wa uwanja wa CCM Mkwakwani Nasoro Makau kulia akitokea msaada wa vifaa vya maji tiririka kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mkoani Tanga (Red Cross)  Ester Wiliam ambavyo vitatumika kuwekwa milangoni kwa ajili ya watazamaji wanaoingia kwenye uwanja huo kushuhudia michezo mbalimbali kuweza kunawa mikono ikiwa ni mapambano dhidi ya Covid 19 kulia ni Mratibu wa Shirika hilo Sada Kombo
 MENEJA wa uwanja wa CCM Mkwakwani Nasoro Makau akinawa mikono mara baada ya kupokea msaada wa vifaa vya maji tiririka kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mkoani Tanga (Red Cross)  Ester Wiliam kushoto ambavyo vitatumika kuwekwa milangoni kwa ajili ya watazamaji wanaongia kwenye uwanja huo kushuhudia michezo mbalimbali kuweza kunawa mikono
  MENEJA wa uwanja wa CCM Mkwakwani Nasoro Makau akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mkoani Tanga (Red Cross)  Ester Wiliam akizungumza
 Mratibu wa Chama hicho Mkoani Tanga Sada Kombo
MENEJA wa uwanja wa CCM Mkwakwani Nasoro Makau kulia akitazama vifaa hivyo mara baada ya kukabidhiwa
 

CHAMA la Msalaba Mwekundu Tanzania Mkoani Tanga (RedCross) kimetoa msaada wa vifaa vya maji tiririka kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini hapa kwa ajili ya kujikinga na Covid 19 kwa watazamaji wanaoingia kwenye uwanja huo kushuhudia michezo mbalimbali.

Makabidhiano hayo yalifanyika kwa Meneja wa uwanja huo Nasoro Makau katika halfa iliyohudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa shirika hilo mkoani Tanga.


Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Meneja Makau alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia vifaa hivyo ambayo vitawekwa kwenye milango mbalimbali ya kuingilia kwenye uwanja huo wakati wa michezo mbalimbali.

Alisema kwamba wana shukuru sana kwa sababu tukio hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali kwa tamko lake michezo imefunguliwa lakini lazima mazingatio yafuatiliwe uwanja na tayari walikuwa na vifaa ambavyo waliviweka ingawa vilikuwa vichache sana


“Kutokana na hilo tunawashukuru Red Cross kwa kuona hilo na ndio maana wameamua kutusapioti kwa kuweka vifaa hivyo kila mlango kwa lengo la kuhakikisha kila mtazamaji anayeingia kwenye uwanja huu ananawa mikono na maji tiririka”Alisema.

Awali akizungumza Makamu Mwenyekiti wa Red Cross Mkoani Tanga Ester Wiliam alisema wameona watoa msaada huo baada ya Rais kuruhusu shughuli za michezo kwa waunge mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Covid 19.

“Tumekabidhi baadhi ya vifaa vya kunawia mikono mashabiki ambao wanakwenda kutazama michezo mbalimbali na tunahaidi kuendelea kushirikiana nao kuweza kupeleka vifaa vyengine”Alisema

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: