ImageRais Magufuli amesema alitengua uteuzi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo na wenzake wawili, kutokana na kutotekeleza maagizo yake huku wakiendekeza malumbano kwa takribani miaka miwili.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Juni 2020, wakati akiwaapisha viongozi wapya – Iddi Kimanta (Mkuu wa Mkoa wa Arusha), Kena Kihongosi (Mkuu wa Wilaya ya Arusha) na Dk. John Pima (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha), Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Mimi saa nyingine nasikitikaga sana unapoona watu uliowateua na ukawaapisha na kuwaamini kwa niaba ya Watanzania, wanapoenda kule hawafanyi kadri ya viapo,.

"Mtakumbuka hivi karibuni nilitengua uteuzi wa wote, sababu katika kipindi cha miaka mwili walikuwa wanagombana tu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Kila mmoja ni bosi anatengeneza migogoro  kwa mwenzake sikufurahishwa, walifanya kazi zao lakini waliniudhi wao kutoshirikiana na kufanya yale ambayo nimewaagiza, sasa nimewateuwa ninyi sitaki yakajitokeze hayo.

"Pale Monduli kuna Migogoro inatengenezwa kwa makusudu. Mfano Mgogoro wa Kanisa na Shule. Wataka Jiji likalipe Milioni 400 ili wajenge Shule.

"Kulikuwa na Mgogoro kwenye Msikiti, kuna kiongozi alikuwa anawahubiri Waislam, Mkurugenzi alipokataa akaonekana mbaya. Mwinyi, Mkapa na Kikwete walikataa, Na Kikwete alijibu kwa Maandishi kukataa. Kwa hiyo msimamo ni ule ule.  Tatizo lile limeletelezwa na mkuu wa mkoa. Kila mmoja anatoa ahadi, tusitoe ahadi ambayo haiwezekani. Nalizungumza hili ili mkuu wa mkoa, Wilaya na DC Msiingilie.

"Kenani wewe ulikuwa Mwenyekiti wa UVCCM na ulikimbiza mwenge mwaka jana, umezunguka nchi nzima na Tanzania unaifahamu. Nina imani hauwezi kushindwa kazi Arusha "


Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema alitaka kuwafuta kazi  Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha na Kamanda wa TAKUKURU Arusha kwa kile alichoeleza ni kufanya shughuli ambazo ziko kinyume na majukumu yao.
 

Hata hivyo amesema, ameamua kuwasamehe kwa sharti la kutorudia tena makosa yao, na kwamba hatosita kuwafuta kazi kama hawatabadilisha mienendo yao.

“Kamanda wa Polisi Arusha na Mkuu wa Takukuru Arusha nilikuwa niwatoe leo, ila nimewasamehe, Sijawasamehe moja kwa moja, najua salamu zitafika. Waambie wakafanye kazi nilizowatuma. Wasimamie sheria sio wafanye kazi zao,” amesema.
Share To:

Post A Comment: