Mkuu wa Wilaya ya Arusha  Mhe Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa Dini Mkoa wa Arusha kudumisha ushirikiano baina yao na serikali,ili kuondoa kero mbalimbali na kusaidiana na  serikali kuhamasisha maendeleo katika MKOA wa Arusha na na nchini kwa Ujumla,ameyasema hayo mapema hii leo akifungua mkutano wa uchaguzi baraza kuu la waislam BAKWATA mkoa wa Arusha katika ofisi za Baraza hilo Arusha.

Kihongosi amesema viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika Taifa hasa katika kuwashauri viongozi na kuliombea Taifa na ndio maana kiongozi mkuu wa nchi aliweka imani kubwa kwao  na kufanya kitendo cha kishujaa kwa kutangaza siku tatu za maomnbi na kuwataka waliombee taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona kitendo kilicho ipa ushindi taifa letu ushindi dhidi ya maambukizi hayo.

Ameongeza kuwa kitendo hicho kiliyashangaza mataifa makubwa kwa kuliona taifa letu lenye kiongozi shupavu linaepukana na vifo vya virusi vya Corona, huku katika mataifa hayo maambukizi na vifo vya wagonjwa wa Corona yakiongezeka kwa kasi.

Amesema kwenye nchi yetu hayo hayakutokea kwa sababu tuna kiongozi makini mwenye hofu ya Mungu na kiongozi anaeshirikiana kikamilifu na viongozi wa dini bila kubagua dini,tunamshukuru kwa kuona kuna umuhimu wa kumtanguliza mwenyenzi Mungu na viongozi wa dini katika majanga yote yanayolikumba taifa letu. 

Ameongezakuwa nchi ya Tanzania tuna bahati ya kumpata Rais na viongozi wakuu wa Serikali wanaopenda mashirikiano na viongozi wa dini,kwahiyo umoja na ushirikiano baina ya viongozi wa Serikali na dini udumishwe na tusikubali awepo wa kuuvunja ushirikiano huu ili uweze kuleta maendeleo na amani katika nchi yetu.

 “Kupitia janga la virusi vya Corona Mwenyenzi MUNGU ametuonyesha ni kwanamnagani Tanzania tuna RAIS bora baada ya mataifa mengine kuamua raia wao wafungiwe yeye aliwataka watanzania wamwombe Mungu na wafanye kazi,tunaweza kusema Tanzania tuna *extra ordinary President* ambae yeye anamaono ambayo viongozi wengine hawakuwanayo Dunia nzima”aliongeza Dc Kenani

Aidha amewataka viongozi watakao chaguliwa wahakikishe wanawaunganisha waumini wao na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili kulikomboa Taifa na uchumi wa familia  kama ilivyo adhima ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli inayolenga kuhakikisha kipato cha Mtanzania kinaongezeka.

Katika mkutano huo wa Uchaguzi Mhe Kenani Kihongosi alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha MH.IDD HASSAN KIMANTA ambapo uchaguzi huo ulilenga kupata wajumbe watakao wakilisha  baraza hilo(BAKWATA) kimkoa katika uchaguzi mkuu wa BAKWATA kitaifa.
Mkutano huo Ulihudhuliwa na KATIBU MKUU WA BAKWATA TANZANIA ,pia ulijumuisha wajumbe 50 kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha ikiwemo mashehe,makatibu,wenyeviti wa baraza hilo halmashauri ya mkoa,mhasibu,jumuiya ya wanawake na viongozi wa juu wa Mkoa pamoja na wajumbe wa kualikwa.
Share To:

Post A Comment: