Mmoja wa wanafunzi katika chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru akiuliza swali kwa Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA walipoenda chuoni hapo kutoa elimu namana ya matumizi sahihi ya Mitandao pamoja na kuwajengea uelewa namna ya kutunza usiri wa faragha zao.
Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru wakifuatilia kile kinachoendelea kutoka mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru walipoenda kuwapatia elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao katika kuadhimisha Haki ya Mlaji
Afisa wa Mawasiliano kutoka TCRA Makao makuu Robin Albert Ulikaye akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Mkoani Arusha juu ya matumizi bota ya mtandao
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA akiandika maswali ambayo waliulizwa na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru mkoani Arusha.

Lucy Mbogoro mtumishi kutoka TCRA akimsikiliza mmoja wa wanafunzi akiuliza swaki kwa Mamlaka hiyo
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya jamii wakiendelea kuwasikiliza watumishi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini walipotembelea chuoni hapo ili kuwapatia elimu namna ya kulinda faragha zao na juu ya matumizi bora ya mtandao
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imeadhimisha siku ya Haki ya mlaji katika chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwakumbusha juu ya matumizi sahihi ya mtandao pamoja na huduma za mawasiliano.
Akizungumza katika na wanafunzi hao Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TCRA) Mhandisi Imelda Salimu alisema kuwa Siku hiyo Haki ya mtumiaji/Mlaji huadhimishwa kila mwaka duniani kote ambapo TCRA inaadhimisha kwa kumlenga mtumiaji wa huduma za mawasiliano
‘’Ni kwamba mtumiaji anapotumia huduma hizi za mawasiliano apate huduma hizo kwa uhakika na na kuhakikisha muda wote huduma hizo zinakuwa bora na zinazofikika wakati wote na utaratibu wa kuzipata haki zake wakati huohuo na wajibu wake kama mtumiaji wa huduma hizo za mawasiliano’’alisema mhandisi Imelda.
Akianisha wajibu na Mamlaka ya Mawasiliano amesema lengo ni kukuza ushindani unaofaa kulinda maslahi ya mtumiaji na watoa huduma za mawasiliano na kuhakikisha kuwa huduma
wanazozipata ni endelevu na zisizo na usumbufu kwa watumiaji
Kwa upande wake Afisa wa Mawasiliano kutoka TCRA Makao makuu Robin Albert Ulikaye amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanazingatia mambo muhimu katika matumizi sahihi ya mtandao kama vile kutokuweka taarifa zao katika mitandao kama vile nywila na anwani zao na kutokujibu jumbe zinazotumwa kwao zinazoulizia taafifa zao bila kujua uhalali.
Awali TCRA iliwaelekeza wanafunzi hao wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru njia sahihi ya kutunza faragha zao pamoja na kufahamu kuwa wanawajibika kuwa na matumizi sahihi ya vifaa vya mawasiliano sambamba na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ikiwemo simu za kiganjani ambapo karibia kila mmoja anayo na anaitumia
Aidha amewataka kutoweka kiwango kikubwa cha fedha kwa muda mrefu ,sambamba na kutokutoa namba zao za siri kwa mtu awae yeyote pia wanapokosea kutuma fedha wahakikishe kuwa wanawasiliana na mtoa huduma za fedha ili aweze kuzirejesha kwa muhusika.
Ulikaye alisema kumekuwa na uelewa mdogo wa watumiaji kuhusu matumizi ya simu janja kutokana na watumiaji kukosa uelewa,hivyo amewataka kuhakikisha wanafunga kurasa zote zinazotumia internet ambazo wamezifungua,mara baada ya kumaliza kuzitumia (log out) kutokupakua bidhaa bila ridhaa kwenye vifaa vyao ili kuhakikisha wakati wote wanakuwa salama
Akizungumza baada ya kupatiwa mafunzo hayo mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Jonatan James alisema kuwa mafunzo hayo aliyoyapata kutoka TCRA ya matumizi bora ya mtandao yamemjenga kiuwezo kwa kuelewa ni vitu gani anachotakiwa kufanya mtandaoni anapoingia kwenye mfumo wa internet.
Vilevile amejua taratibu za kukata rufaa au anapokuwa na malalamiko yake kuyapeleka TCRA hivyo elimu hiyo imemjenga kiakili na kuweza kujitambua na kuongeza umakini ili kulinda faragha yake.
Mwisho
Post A Comment: