Mwenyekikiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Arusha Ndugu Omary Bahati  Lumato amefanya ziara ya kikazi ya kukagua uhai wa Jumuiya ya vijana katika wilaya ya Longido.

Ambapo katika ziara hiyo akiwa ameambatana na Katibu Hamasa na Chipukizi Ndugu Edson Ndyemalila amewataka viongozi wa UVCCM kujenga uhusiano mzuri na viongozi wa selikali ili kuwaondolea kero wananchi na kuwaharakishia maendeleo.

Pia Ndugu Lumato amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuwaondolea kero wananchi na kuwaharakishia maendeleo, vijana wasikubali dhamira hii njema kukwamishwa au kupotoshwa.
Aidha aliendelea kuwahimiza viongozi wa UVCCM Wilaya ya Longido na mkoa kwa ujumla kuhakikisha wanaingiza wanachama wapya.

Aidha amewakumbusha vijana kuheshimu utaratibu wa kupata uongozi katika nafasi za ubunge na udiwani kama ilivyoelekezwa kwenye kanuni za uchaguzi na kuwa Chama cha Mapinduzi ni cha wanachama na hakuna mtu mwenye hati miliki ya chama.

Sambamba na hapo pia mwenyekiti huyo amewakumbusha vijana kugombea katika nafasi za ubunge na udiwani muda ukifika Kwani kugombea ni haki ya kila mwanachana lakini kuteuliwa ni fursa, pia amewakumbusha vijana kuwa ni wajibu wa kila mwanachama kumtafutia kura Mgombea atakayeteuliwa na Chama Cha Mapinduzi.

IMETOLEWA NA
EDSON NDYEMALILA
KATIBU HAMASA NA CHIPUKIZI UVCCM MKOA WA ARUSHA
Share To:

msumbanews

Post A Comment: