Madawati yaliyotolewa msaada na aji ya kunywa wanafunzi kutoka kampuni ya Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd
Fliji lililotolewa msaada na kampuni ya Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd ajili ya kuhifadhia maji ya wanafunzi
Na Heri Shaaban
MSTAKIHI meya wa halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amepokea msaada wa madawati 25 na fliji za maji ya kunywa wanafunzi kutoka kampuni ya Tanga Pharmaceutical and Plastic Ltd kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu.
Madawati hayo yamepokelewa leo katika shule ya msingi Mtakuja manispaa ya Ilala.
Akizungumza baada kupokea msaada huo Meya Kumbilamoto ameipongeza kampuni hiyo kwa msaada huo katika kuisaidia serikali ya awamu ya tano.
"Naipongeza kampuni hii kwa juhudi za kuisaidia elimu nawaomba wanafunzi wa shule hii na Wilaya ya Ilala kwa ujumla kuzingatia elimu kwani elimu ni ufunguo wa maisha " alisema Kumbilamoto.
Alisema kampuni hiyo inatarajia kuleta madawati mengine 25 kwa ajili ya shule hiyo na kufikia jumla ya madawati 50.
Aidha katika hatua nyingine meya Kumbilamoto amewapongeza Walimu wa manispaa ya Ilala na afisa elimu msingi kufuatia Maniapaa hiyo kufanya vizuri matokeo ya darasa la nne mwaka 2020 kushika nafasi ya pili kitaifa.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas ameipongeza shule hiyo kufanya vizuri matokeo ya darasa la nne.
Afisa elimu Thomas katika halmashauri ya Ilala siri kubwa ya ufalu mzuri ni mazingira mazuri ya shule hizo na walimu wazuri katika shule zake.
Meneja mwajiri wa Tanga Pharmacetical and Plastic Ltd Stephen Kagoso alisema kampuni hiyo Wilaya ilala ina Miaka 15.
Kagoso alisema wao kama wawekezaji wameguswa katika juhudi za kumsaidia Rais magufuli kukuza Elimu nchini.
Post A Comment: