Madaktari na wauguzi wa kituo cha afya Malangali Katika Halmashauri ya Mufindi wakiwa wamefanikiwa kufanya upasuaji salama wa kwanza
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa inaendelea kutekeleza ilani ya CCM leo kituo cha afya Malangali kimefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza salama wa kihistoria .
Akizungumza baada ya zoezi hilo kubwa na la mafanikio kwa sekta ya afya mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi Netho Ndilito alisema kuwa kituo hicho ni miongoni mwa vituo 352 vya Afya Tanzani vilivyoboreshwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Msgufuli .
Hivyo alisema jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kwa Halmashauru ya Mufindi wanapongeza sana hasa baada ya kilio chao kupatiwa majibu .
" kwa mara ya kwanza kituo cha afya Malangali kimeanza kutoa huduma ya uasuaji baada ya Rais Dkt.John Magufuli kutupatia vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Tsh milioni 204"
Alisema Januari 21 mwaka huu majira ya saa tano usiku timu ya wataalamu madaktari na wauguzi walifanya upasuaji wa kwanza na wa kihistoria wa mama mjamzito katika kituo hicho cha Afya cha Malangali.
Hivyo alisema ni furaha kubwa kwa serikali ya wilaya ya Mufindi chini ya mkuu wa wilaya Jamhuri Wiliam ,madiwani wote kupitia mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Festo Mgina kwa utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo kwa pamoja na kupata matokeo mazuri kupitia kituo hicho kwa kupata mwanafamilia mpya mtoto wa kike aliyepatikana kwa upasuaji salama .
"Shukrani za pekee kwa Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt.John pombe Magufuli kwa kuendelea kugusa maisha na nafsi za Watanzania zawadi kubwa kwake ni kuendelea kumuombea zaidi "
Alisema Halmashauri hiyo na wananchi wake wameendelea kunufaika na utendaji kazi mzuri .
" Tukishindwa kumshukuru kwa vinywa vyetu wenyewe kwa Rais Dkt John Magufuli anayeokoa maisha yetu basi tujiandae kuhukumiwa ahela, mimi na Wananchi wa Halmashauri ya MUFINDI tunakushukuru sana sana mheshimiwa Rais kwa kuendelea kujali, kutambua na kuthamini maisha yetu lakini pia kutuletea Maendeleo makubwa na ya kihistoria katika Halmashauri yetu ya Mufindi Mungu akubariki sana"alisema Ndilito
Post A Comment: