Wanamitindo mbali mbali Duniani wakiwa na mwenyeji wao Flaviana Matata katika Hifandhi ya Taifa ya Serengeti 
Wanamitindo hao wakipiga picha ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti 


MWANAMITINDO maarufu Duniani Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Marekani,Flaviana Matata ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii akiwa ameambatana na Wanamitindo wenzake kutoka Marekani.

Flaviana Matata  ameongozana na wanamitindo  Shelby Colemans, Daniella Evans na Awa Florence Mafany ambao kila mmoja anafanya shughuli za mitindo huku wakiwa na wafuasi wengi kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Flaviana Matata akiwa na rafiki zake hao, wameweza kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya Serengeti ikiwemo wanyama mbalimbali sambamba na uzuri wa Hifadhi hiyo ambayo ni kubwa hapa Nchini.

Ziara hiyo ya kuambatana na Wanamitindo hao ni kwa lengo la kuona vivutio vya utalii vilivyoko katika hifadhi na kuvitangaza.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: