.
Watalii kutoka nje ya Tanzania wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Wanahabari wa mikoa ya Iringa na Mbeya wakiwa safarini kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti 
Basi lililotumiwa na wanahabari hao 
Vikapu vilivyotengenezwa na malighafi kutoka Njombe 
 Na Francis Godwin, Serengeti
Wadau  wa Utalii katika hifadhi ya  Serengeti wilaya ya Serengeti mkoani Mara amewataka askari wa usalama barabarani katika mikoa yenye hifadhi za Taifa (TANAPA) na vivutio vingine vya utalii kuwa wadau namba moja wa uhamasishaji Utalii nchini kwa kutowasumbua madereva wa magari yanayosafirisha watalii.

Akizungumza na wanahabari kutoka mkoa wa Mbeya na Iringa waliokuwa katika ziara ya kikazi ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti jana Johnson Ndilakwe ambae ni dereva wa magari ya kubeba watalii .

Alisema kuwa wanapokuwa na watalii hasa kutoka nje ya  Tanzania baadhi ya mikoa kumekuwepo na usumbufu mkubwa wa askari wa usalama barabarani na lugha kali wanazitumia kumhoji dereva zimekuwa zikiwatisha watalii.

"Ujue kabisa huyu mtalii toka nje anapokuja kutembelea Hifadhi zetu amekuwa akiliongezea kipato Taifa na ziara yake ni ya Utalii hahitaji usumbufu sasa pale askari wa usalama barabarani wanapoonyesha kuwasumbua madereva wao suala hilo linawakwaza sana"alisema

Zipo baadhi ya njia za mikoa inayoongoza kwa kusumbua madereva wa magari ya watalii ila kwa njia ya Singida ,kuelekea Mwanza askari wake wamekuwa waungwana sana na ni wacheshi sana kwa madereva wa magari ya watalii kwa ujumla wao .

Hivyo alishauri jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kujifunza kwa askari wa mikoa wa njia za kuelekea Hifadhi za Kaskazini jinsi wanavyoonyesha furaha na upendo kwa watalii.

Kwani alisema iwapo watalii hawatapokelewa vizuri na askari hao dosari inabebwa na nchi nzima kwa watalii hao kuchukia kufika kutembelea Hifadhi zilizopo mikoa yenye usumbufu .

Ndilakwe alisema kwa sasa serikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa akielekeza nguvu nyingi katika kutangaza vivutio vya utalii na Hifadhi mbali mbali zikiwemo za mikoa ya kusini na nyingine ila jitihada hizo zitakwama kufanikiwa kama watalii hawatapokelewa vizuri .

Alisema askari wa usalama barabarani wanapaswa kutambua faida kubwa ya watalii hao katika Hifadhi zetu kwani wamekuwa wakiliongezea Taifa uchumi wake.

Pia alipongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha hadhi za Hifadhi za Taifa nchini huku akishauri suala la miundo mbinu hasa kipindi cha masika kutazamwa kwa jicho la tatu .

Alisema mfano Hifadhi ya Taifa ya  Serengeti wageni wengi wamekuwa wakipenda kupelekwa katika Hifadhi hiyo kutokana na ubora wake ila baadhi ya maeneo hali ya miundo mbinu ya kuelekea Hifadhi si mizuri sana.

Hivyo alizitaka Halmashauri zinazozunguka Hifadhi hiyo kutenga bajeti ya uboreshaji wa miundo mbinu kwani kupitia watalii hao Halmashauri mapato yake ya ndani yamekuwa yakiongezeka .

Mwanahabari Laundence Simkonda kutoka mkoa wa Mbeya akielezea  ziara hiyo ya utalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti alisema ziara hiyo imekuwa na tija kubwa kwao kwani wataitumia ziara hiyo kufikisha kwa umma  jinsi ambavyo wanaweza kunufaika moja kwa moja na Hifadhi za Taifa kwa kujikita katika shughuli za bidhaa za Kitalii .

Alisema mji wa Serengeti na  maeneo mengine ambayo yamezungukwa na Hifadhi za Taifa nchini yakiwemo ya Hifadhi za Kusini yana nafasi ya kutumia fursa ya kuwa karibu na Hifadhi hizo kwa kufanya shughuli za biashara za kitalii.

Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Rebeca Msambuse alisema kuwa Halmashauri hiyo ipo mkakati wa uboreshaji wa miundo mbinu inayozunguka hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kuwavutia watalii zaidi kuendelea kutembelea hifadhi hiyo ambayo ni hifadhi yenye watalii wengi zaidi hapa nchini.

Pasipo kutaja kiwango cha fedha zilizotengwa na urefu wa barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami na changarawe alisema mpango wa uboreshaji wa miundo mbinu unategemewa kuanza kutekelezwa mwaka huu

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: