Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndugu Lootha Ole Sanare ,ameupongeza uongozi wa  Wilaya ya Mvomero Kwa usimamizi makini wa miradi ya maendeleo .

Kauli hiyo ya Mkuu wa mkoa ameitoa hii leo alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo kukagua ujenzi wa wodi ya kinamama na watoto na ujenzi wa shule ya sekondari ya kumbukumbu ya hayati Edward moringe sokoine  yote yakiwa katika makao makuu ya Wilaya hiyo.

Nimetembelea na kukagua miradi hii nawapongeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Kwa usimamizi makini wa miradi hii  kweli mmeitendea haki Fedha ya serikali hivyo naomba muongeze ngivu zaidi ili muweze kukamilisha sehemu zilizo bakia ili hutuma zianze kutolewa .

Aidha Mkuu wa Wilaya Mwl Muhamed Utaly amesema wameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa na atahakikisha wanayasimamia kikamilifu ili  sehemu hizo zilizo bakia ziweze kukamilika Kwa asilimia mia moja wananchi waweze kupata huduma.

Naye mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Florent Kyombo amesema kuwa kulikuwa na changamoto ndogo zilizokuwa zinakwamisha ukamilishwaji wa miradi hiyo lakini kwa sasa wameshazitatua na kumuhakikishia mkuu mkoa kuwa miradi hiyo itakamilika kwa muda waliokubaliana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: