WAZIRI wa Nishati Dkt Medrad Kalemani kushoto akionyeshwa kitu ni Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo hicho
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela kulia akimuonyesha kitu Waziri wa Nishati Dkt Medrad Kalemani kushoto wakati wa ziara yake kwenye kituo hicho
Sehemu ya mitambo iliyopo kwenye kituo hicho cha kuzalisha umeme
Meneja wa Tanesco mkoa wa Tanga Julius Sabu kulia akipitia taarifa wakati wa ziara hiyo
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema kwamba dhamira ya serikali ni kuhakikisha
mtambo wa kuzalisha umeme wa hale unarejea kwenye hali yake ya kawaida ili
uweze kutoa megawatts 21 kama ilivyosanifiwa na kuanza kufanya kazi mwaka 1964.
Dkt
Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha kuzalisha
umeme cha Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga ambapo pia alitembelea mgodi wa
kufua umeme.
Akiwa
kwenye kituo hicho Waziri Kalemani alisema kwamba ametembelea mradi huo kwenye
maeneo makubwa mawili ya mashine na trasfoma huku akieleza kwamba kwenye
mashine mbili ambazo zipo eneo hilo hazifanyi kazi kwa sasa maanake hatupati megawati
hata moja kutoka kwenye mtambo huo.
Alisema
kwamba ingawa mtambo mmoja unafanyiwa marekebisho kwa maana ya kufungwa vifaa
na wataalamu hivyo watahakikisha unakamilika na tayari alikwisha kutoa
maekelezo kazi hiyo ikamilike ili megawatts 10.5 zirejee.
“Hapa
katikati mlikuwa mnapata megawatts 8 zilikuwa hazifiki hata kumi ..wakati huu
matengenezo makubwa yanafanyika hivyo ni matumaini yake kwamba hata mkandarasi
ambaye anatafutwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya mitambo yote miwili
utafanyika haraka “Alisema Dkt Kalemani
Hata hivyo
alisema lazima wahakikisha wanakuwa na umeme wa kutosha ambao utapatikana
kwenye mradi huo ambao ni wa miaka mingi kwani ulijengwa mwaka 1964 hiyo
mitambo kila wakati lazima ifanyiwe ukarabati hasa wakati unapopita.
“Mwaka juzi
nilipita hapa na kutoa maekelezo kutokana na kuwepo dalil za mitambo
iliyochakaa nikawaambia muanze utaratibu wa kufanya marekebisho ya mitambo yote
wakati wa ziara yangu kupita kwenye mitambo ni kujihakikisha umeme unapatikana
na wa uhakika”Alisema
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhandisi Mkuu wa Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Pangani Hydro System Jackline Mtolela alimueleza Waziri Kalemani kwamba hali ya mitambo iliyopo
kwnye kituo hicho ni chakavu ya mwaka 1964ina hitaji matengenezo makubwa.
Alisema
kutokana na hali hiyo hivi sasa wapo kwenye mchakato wa kupata wakandarasi ili
waweze kufanya ukarabati kwani kwa sasa wana uwezo wa kuzalisha megawatts 10.5
kwa mashine moja ila kutokana na uchakavu wa mashine wanazalisha megawatts 8
lakini mashine ipo kwenye matengenezo.
Post A Comment: