Na Amiri kilagalila­-Njombe
Aliyekuwa mwenyekiti  wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa pili mkoa wa Njombe Edwirn Enosy Swale  (wakili) baada  ya wa awali ndugu Fakih Lulandala kukihama chama hicho mwaka 2018 na kujiunga na chama cha mapinduzi naye pia hii leo amejiuzulu uenyekiti wa chama hicho na kujiunga na CCM.

Akizungumza mara baada ya zoezi la kupokelewa,kuapishwa na kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi katika ofisi za CCM wilaya ya Njombe amesema amefanya maamuzi hayo kutokana na juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuleta maendeleo nchini.

“Mimi kama kijana nimeamua kwa dhati kutumikia nchi yangu katika chama ambacho kwa sasa kimekuwa na muelekeo wa kusaidia wananchi,na nitoe wito kwa vijana wote nchini na watanzania kwa ujumla wake,tusije tukapoteza fursa ya kutokumtumia Magufuli kuipeleka nchi yetu katika hali neema”alisema Swale

Katika hatua nyingine chama cha mapinduzi kimempokea aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) jimbo la Lupembe Msafiri Peter Mpolo,ambaye amesema ameamua kuhama chama hicho kutokana na kuto kuwepo kwa ajenda za kusimamia kwa sasa.

“Tumeona hakuna sababu ya kuendelea chama cha upinzani kutokana na mambo makubwa ambayo yamefanywa na serikali kwa sasa,ukienda Makete utaona barabara zinavyojengwa,watumishi wamekuwa na nidhamu kubwa,hizo ndio ajenda tulizokuwa tunasimamia lakini leo hii nikibaki Chadema nitasimamia nini”alisema Msafiri Peter Mpolo

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha na kuwakabidhi kadi wanachama hao mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Edward Mgaya,amemtaka Swale kuunganisha nguvu zake pamoja na mbunge wa jimbo la Lupembe Jorum Hongoli  ili kufikisha maendeleo katika jimbo hilo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: