NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KIJANA
anayeishi kwa msaada wa mashine ya Oxygen ili kumuwezesha kupumua, Bw. Hamad
Awadhi amelishukuru Shirika la Umeme Nchini TANESCO kwa kumpunguzia mzigo wa
gharama za umeme kwa kumlipia bili ya umeme wenye gharama ya Shilingi Milioni
1,500,000/=/.
Kijana
huyo ambaye anaishi eneo la Ukonga Majumba Sita jijini Dar es Salaam, alisema
madaktari walimueleza kuwa mapafu yake yameharibika na hawezi kuishi bila ya
kutumia msada wa mashine ya oxygen na kwamba mashine hiyo inayotumia umeme,
amekuwa akilipia bili ya umeme shilingi 45,000/= kila wiki.
“Kwaniaba
ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, tumeguswa baada ya kupata
taarifa za maradhi yanayokusumbua, tumekuja kukupa pole na kukuombea kwa
Mwenyezimungu, lakini sisi kama Shirika linalotoa huduma katika jamii, tumeona tunaweza kufanya kitu kidogo hata kama si kumaliza tatizo basi hata
kupunguza ili uone kwamba licha ya matatizo yanayokukabili jamii iko nawe na
inakujali.” Kaimu Meneja Uhusianbo wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Bi. Leila
Muhaji alimueleza Bw. Awadh, wakati alipoambatana na Meneja wa TANESCO Mkoa wa
Ilala Mhandisi Sotco Nombo kumjulia hali na kumpatia taarifa ya msada kutoka
TANESCO.
Bi.
Leila alisema, “TANESCO tunafanya kazi ya kutoa huduma ya umeme, tutahakikisha
unapata umeme bila kuwaza kwa muda w amiezi 6, tutatoa shilingi Milioni
1,500,000/= ili isaidie katikakipindin hicho.” Alisema Bi. Leila.
Bi.
Leila alisema, sambamba na kulipia gharama hizo za umeme TANESCO pia baada ya
kupata ridhaa ya mwenye nyumba anamoishi Bw. Awadhi, itamfungia mita yake pekee
ya umeme na kumuwekea mfumo wa umeme utakaomuwezesha kujitegemea yeye mwenyewe
na hivyo kumpunguzia mzigo wa gharama za kulipia bili ya umeme.
Aidha
Kaimu Meneja Uhusiano huyo wa TANESCO, alisema Shirika pia limezingatia ombi
lake la kusaidiwa fedha za kumuwezesha kupatiwa matibabu nje ya nchi.
“Sisi
kama TANESCO tutachangia shilingi milioni 10 ili kuchangia matibabu yako, fedha
hizi hazihusiani na kulipia gharama za umeme hizi fedha ni za kuchangia matibabu
yako na tutaziwasilisha, leo tumeona tufike tukupe pole na tukueleze jinsi tulivyoguswa
na taarifa ya maradhi yanayokusibu.” Alifafanua Bi. Leila Muhaji.
Aidha
Meneja wa TANESCO Mhandisi Sotco Nombo alisema, baada ya kupata ridhaa ya
mwenye nyumba TANESCO itagharimia gharama zote za ufungaji wa mita, na kufunga
mfumo wa umeme utakaomuwezesha kutumia umeme wa kwake peke yake bila ya
kuingiliana na wakazi wengine katika nyumba hiyo.
“Kama
mnavyojua mpendwa Rais wetu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza suala la
uzalendo miongoni mwa watanzania, na sisi tumeona tuungane na watanzania
wenzetu ili kumsdaidia Mtaznania mwenzetu anayesumbuliwa na maradhi haya.”
Alisema Mhandisi Nombo na kuongeza
“Tutamuwekea
umeme wa peke yake, kama mnavyoona hapa kuna wapangaji zaidi ya watano na wote
wanatumia mita moja na hakika matumizi lazima yatatofautiana na kama mnavyoona
matumizi ya Awadhi sio makubwa kiasi hicho cha kutumia kiasi cha shilingi
45,000 kwa wiki, tumeona tufungue mita ya kwake pekee tunachofanya kwa sasa ni
kuwasiliana na mwenye nyumba ili kupata ridhaa yake.” Alifafanua Mhandisi
Nombo.
Akitoa
shukrani baada ya taarifa hiyo kutoka TANESCO, Bw. Awadhi alisema “Umeme ndio maisha
yangu, ndio Mungu wangu wa pili ingawa Mungu hashirikishwi, siwezi kufananisha
na Mungu lakini mimi bila umeme ndio basi tena, mashine hii inatumia umeme
masaa yote.” Alisema Bw. Awadh.
Aliishukurui
TANESCO kwa msada huo mkubwa na kutoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza
ili kumsaidia.
Kaimu Meneja Uhusianbo wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Bi. Leila
Muhaji (Kulia) akiwa na Meneja wa TANECO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo, (matikati), akizungumza leo Septemba 5, 2019 mbele ya kijana Hamad Awadhi anayeishi kwa msada wa mashine ya oxygen kumsaidia kupumua wakati walipomtembelea nyumbani kwake Ukonga Majumba Sita jijini Dar es Salaam.
Kijana Hamad Awadhi akiwa na mipira iliyounganishwa kwenye mashine hiyo.
Kijana Hamad Awadhi akiwa ameketi na mshine yake pembeni.
Hizi ni mashine mbili tofauti, moja iliyo mbele ni mashine ya Oxygen inayotumia umeme ambayo humsaidia kupumua wakati aanapopata tabu ya kupumua mwenyewe. na nyuma ni mtungi wa oxygen ambao nao huutumia wakati ambapo hakuna umeme.
Post A Comment: