Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa amewataka waandishi wa habari nchini kuongeza kasi ya kuripoti kwa usawa habari za jinsia na uchaguzi kulingana na umuhimu wake katika jamii.

Akiwasilisha mada kuhusu uandishi wa habari za uchunguzi na masuala ya jinsia kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kutoka Visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar), Gasirigwa alisema kwa muda mrefu habari za aina hiyo hazipewi kipaumbele ikilinganishwa na habari nyingine.

“Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandaa na kuripoti habari za uchunguzi na jinsia ili kuweka usawa wa kutetea wanawake katika jamii” alisisitiza Gasirigwa.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo waliishukuru taasisi ya MISA Tanzania kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuitumia vyema elimu waliyoipata ili kuboresha utendaji kazi wao huku wakiwa mabalozi wazuri kwa wenzao.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia Agosti 16 yalifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Paradise iliyopo mjini Unguja yameandaliwa na taasisi ya MISA Tanzania kwa kushirikiana na ile ya VIKES ya nchini Finland na kushirikisha jumla ya waandishi wa habari 25.
 Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akifafanua jambo.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo hayo kupitia makundi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: