Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa "Tumepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa kuhusu Ajali ya Moto iliyotokea leo Morogoro."

"Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro tunaendelea kuhakikisha majeruhi wa ajali hii wanapata huduma za matibabu haraka!

"Bohari ya dawa wapo njiani kupeleka dawa, vifaa na vifaa tiba vinavyohitajika haraka kwa cases za burn kama vile fluids, strong analgesics, Tetanus toxoid, burn creams, bed credos, gauzes, giving sets, urine bags, catheters kwa ajili ya kuhudumia majeruhi."

 Aidha Katibu Mkuu Afya Dkt. Zainab Chaula, Mganga Mkuu wa Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wapo njiani kwenda Morogoro ili kuongeza nguvu ya kuhudumia majeruhi.

Ninawaombea majeruhi nafuu ya haraka. Pia ninatoa pole kwa ndugu, jamaa waliopoteza wapendwa wao. Inaelezwa kuwa Idadi kubwa ya watu wanahofiwa kufa moto baada ya gari la mafuta lililopata ajali kuwaka moto maeneo ya Msamvu, mkoani Morogoro.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: