Serikali imesema kuwa haitakuwa tayari kuona rasilimali za nchi yetu zinatoka hapa nchini badala ya kunufaisha wananchi wa Tanzania zina kwenda kuzinufaisha serikali za nchi zingine .

Naibu Waziri Wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Abdalla Ulega  ameyasema hayo Leo wakati akiongea na wafugaji na wafanyabiashara Wa wilayani Longido  wakati alipofanya ziara ya kukagua na kujionea  miradi mbalimbali ya Mifugo pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji na wafanyabiashara Wa Mifugo

Alisema kuwa serikali haitamfumbia macho mfugaji yeyote ambaye atatorosha Mifugo na kupeleka nje ya nchi kwani atakuwa anapoteza mapato makubwa ya nchi ,kwani atakuwa amekwepa kulipa tozo mbalimbali ikiwemo kodi ya serikali

Alisema kuwa katika kuthibiti hili serikali imepiga hatua kubwa katika kuzibiti utoroshwaji Wa Mifugo kwenda nje ya nchi kwani hadi sasa wameweza kuweka ulinzi mkali wa askari polisi katika mipaka yetu ambapo amebainisha kuwa  kwa sasa utoroshwaji Wa Mifugo umepungua kwa asilimia 90% hali iliosababisha makusanyo kupanda kutoka milioni sita kwa Siku kwa kipindi  hakuna walinzi na kufikia makusanyo ya shilingi milioni tisa kwa Siku  kwa kipindi ambacho askari Polisi wapo

"Askari polisi hawa wanaolinda mipaka yetu wamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza utoroshwaji Wa mifugo  Nana penda kusema tutaongeza bajeti kwaajili ya kuwalipa askari hawa kwani wanafanya kazi vizuri"

Aidha Naibu Waziri alitoa agizo kwa halmashauri zote hapa nchini kuweka mizani za kupimia uzito ng'ombe katika minadani yote ili kuweza kupima mifugo yao na sio kuuza kwa kukadiria kilo hii itasaidia kumnufaisha mfugaji na sio mfanyabiashara tu.

"Hichi kitendo cha kukisia uzito Wa ng'ombe serikali hauutaki kwani unamuumiza sana mfugaji,kwani anakuwa anauza mfugo wake kwa hasara na anakuwa anamnufaisha mfanyabiashara na mfugaji anadidimia kitu ambacho serikali atukubali kumuona mfugaji ananyanyaswa ,kwa kuzulumiwa serikali yetu inataka kumuinua mfugaji na sio kumdidimiza ,na serikali yetu mnajua inatetea wanyonge" alisema Ulega

Aidha alisema kuwa serikali itawapa Elimu ya kutosha kuhusiana na tozo na hasara za utoroshwaji Wa Mifugo  ili wafugaji hao wasiendelee kutorosha Mifugo hiyo,kwani imebainika kuwa wafugaji wengi hawana Elimu ya kutosha ya sheria za utoroshwaji Wa mifigo,uku akibainisha kuwa iwapo mfugaji  atakamatwa anatorosha Mifugo sheria Kali itafuatwa ikiwemo kupelekwa mahakamani pamoja na kulipa faini .

 Kwa upande  wananchi  hao walitumia muda huo kuomba serikali kuwapa kipaumbele cha kuuza Mifugo yao katika soko la kimataifa linalotarajiwa kufunguliwa katika Kijiji cha  Olendeki kilichojengwa karibu na Mpaka Wa Namanga uliopo wilayani Longido mkoani hapa.

Nae mbunge Wa jimbo la Longido Steven Kiluswa aliomba serikali kuwapunguzia tozo wanazolipia Mifugo kwani iwapo watapunguziwa ,wataacha kabisa kutorosha Mifugo  nafedha zitaingia serikalini na mapato ya nchi yataongezeka ,aidha pia aliomba serikali kuanda semina za kuwaelimisha wafugaji juu ya Elimu ya kodi pamoja na tozo wanazolipa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: