Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Agosti 10, 2019.
Majaliwa akiongozana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako (kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salam, Utawala, Profesa David Mfinanga (kushoto) wakati alipoingia katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Agosti 10, 2019. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Niboye.
Majaliwa akisoma hati ya kiwanja ambacho kitajengwa Ofisi ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kilichopo eneo la Mtumba jijini Dodoma kilichotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kushoto) Agosti 10, 2019 wakati Waziri Mkuu alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TAHLISO katika Ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Niboye.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agosti 10, 2019.
Majaliwa akihutubia wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agosti 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post A Comment: