Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Tarehe 17 Juni
2019 akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu amepata fursa ya kumtembelea
muwekezaji mzawa wa kusindika Nafaka Bw Deogratius Kumalija katika
Wilaya ya Busega.
Akiwa
kiwandani hapo Mhandisi Mtigumwe alipata maelezo kutoka kwa mmiliki
huyo kuwa ameamua kujikita katika usindikaji wa mazao ya Nafaka kutokana
na fursa iliyopo katika kuongeza thamani ya mazao hayo hususani mahindi
na Mpunga.
Bw
Kumalija aliendelea kusema kuwa kiwanda hicho cha Mpunga kina uwezo wa
kukoboa Tani 28 kwa siku na alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kupanga
madaraja ambapo kiwanda cha kusaga Mahindi kipo katika ujenzi na punde
kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusaga tani zaidi ya 30 za mahindi
kwa siku.
Alisema kuwa Viwanda Hivyo vitasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo na kuondokana na nchi kuendelea kuuza mazao ghafi.
Kadhalika,
Mhandisi Mtigumwe alimpongeza muwekezaji huyo kuwa aendelee na
uwekezaji huo pia Serikali imekuwa ikisisitiza kuyaongezea thamani mazao
ya Kilimo.
Hivyo
mwekezaji kama Bw Kumalija anatimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozw ana mHe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Sera ya Viwanda.
Hata
hivyo kwa kuwa na Viwanda kama hivyo vitaongeza ajira na kuhamasisha
wakulima kulima wakiwa na uhakika wa mazao yao na kuyaongezea thamani.
MWISHO.
Post A Comment: