Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Profesa, Rudovick Kazwala, akifundisha kwa vitendo namna ya kutumia Vifaa vya kitaalam vya Kinga Binafsi, wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
Baadhi
ya wataalamu
wa sekta za Afya kutoka Mkoa wa Songwe
na Mbeya kwa Halmashauri zilizopo mipakani wakiwa wamevaa vifaa vya Kitaalamu
vya Kinga Binafsi, wakati wa Mafunzo
hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na
Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja,
tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
Mratibu wa Kitaifa, Dawati la Afya moja, lililopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akisisitiza umuhimu wa sekta za Afya kushirikiana wakati wa mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa wataalamu wa sekta za Afya kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga akisisitiza umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja wakati wa mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa wataalamu wa sekta za Afya kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe
Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Niwael Mtui, akifundisha namna ya kudhibiti magonjwa ambukizi maeneo ya mipakani wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, wakiwa katika makundi ya majadiliano wakati wa mafunzo ya Kuimarisha Udhibiti wa magonjwa ambukizi kwa kutumia Dhana ya Afya moja kwa maeneo ya mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
Mwezeshaji
wa Mafunzo ya kuimarisha
udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Swai, akifundisha namna ya kudhibiti magonjwa
ambukizi maeneo ya mipakani, wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za
Afya kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya
katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani
Songwe.
Dhana ya Afya moja
ambayo hujikita katika kujumuisha
sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta
hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya ya
Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie
dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama
ambayo hutokea mara kwa mara katika
maeneo ya mipakani kutokana na kuwepo kwa mwingiliano mkubwa kati ya watu na wanyama katika mazingira yao.
Pamoja
na Mwingiliano
huo wenye faida kubwa kiuchumi lakini pia unasababisha kuenea kwa
vimelea kwa uharaka zaidi na kusababisha magonjwa
kwa binadamu, wanyama na mimea katika mazingira yao, hivyo ili
kuimarisha Afya
ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),
pamoja na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wamewapa
mafunzo
wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika Halmashauri za Mkoa wa
Mbeya na
Songwe zilizo mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa
ambukizi kama
vile Ugonjwa wa Kimeta kwa kutumia Dhana
ya Afya moja.
Akiongea wakati wa
kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 29 Aprili hadi,tarehe 3 Mei,
2019, Mkoani Songwe, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali
Jimmy Matamwe, ambaye aliwakilishwa na Mratibu Kitaifa, Dawati la Kuratibu Afya
Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka,
alibainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni
agenda ya dunia nzima. Aidha, alieleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika
maeneo ya mipakani ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri
kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia
nchi, utandawazi, ongezeko la mahitaji
ya maji na chakula.
Awali akiongea katika
mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga
alibainisha kuwa sekta za Afya
zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu
kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhri kwa wakati. Aidha alibainisha
kuwa vimelea vingi vinavyo sabababisha
magonjwa kwa binadamu asilimia (60%) vinatoka
kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi yanatokea pale binadamu
anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari, hivyo Afya moja ikitumika
maeneo ya mipakani itasaidia kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi
yanayotokana na shughuli za mwingiliano wa wanyama na binadamu zinazofanyika
sana maeneo ya mipakani.
Katika kuhakikisha watalaam
hao kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana
hiyo katika kudhibiti magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa
uwezo wa namna ya kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile
ugonjwa wa Kimeta, pindi unapotokea maeneo ya mipakani, Namna ya kuunda vikosi
vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa kufuatilia na
kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja, pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga
Binafsi vya Kitaalamu.
Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya
Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya
moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya
Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya
moja kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa
(FAO) waliandaa na kuratibu mafuzo hay
Post A Comment: