NA HERI SHAABAN
JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA imewataka wananchi wa wilaya hiyo kutunza mazingira yao na kushiriki usafi.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo Katibu wa Elimu,Malezi,Mazingira wilaya ya Ilala Wilson Tobola,wakati wa madhimisho ya Wiki ya Wazazi Wilaya ya Ilala ambapo wilaya hiyo wameadhimisha kwa usafi machinjio ya Mazizini Jimbo la Ukonga wilayani Ilala.
"Mimi Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala tunadhimisha wiki ya Wazazi katika wilaya yetu Jumuiya hii ya Chama cha Mapinduzi imetimiza miaka 64 hizi kazi tunazofanya ni sehemu ya utekelezaji wa ilani "alisema Tobola
Tobola alisema moja ya kazi inayosimamia Jumuiya ya Wazazi suala zima la usafi na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ya wananchi wao.
Alisema kama EMAU Wilaya ya Ilala katika Jumuiya ya Wazazi wanasisitiza suala zima la utunzaji wa mazingira na kushiriki usafi kwa vitendo ndani ya wilaya ya Ilala.
Amewataka wananchi kutunza mazingira yao ili wasiharibu vyanzo vya maji kwani maji ni uhai.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Lucas Rutainurwa, mgeni rasmi Katibu wa Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Geofrey Robart na Viongozi wa Kamati ya Utekelezaji walikabidhi vifaa vya Usafi na sabuni kwa Wanawake Wajawazito katika Zahanati ya Serikali MONGOLANDEGE.
Akizungumza katika zahanati hiyo ya serikali mara baada kukabidhi msaada huo Mwenyekiti LUCAS aliwataka wananchi wa wilaya ya Ilala kuwa na imani na Chama cha Mapinduzi ambacho kinatekeleza Ilani.
Lucas alisema dhumuni la ziara hiyo ni kusherehekea sikukuu ya siku ya Wazazi madhimisho ya wilaya pia jamii iweze kuona kazi za Jumuiya hiyo moja ya jukumu lake kusimamia usafi.
Akielezea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu amewataka wananchi kukiamini chama cha Mapinduzi CCM kuchagua viongozi ambao wataweza kutatua changamoto zao.
Naye Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Geofrey Robart alisema kauli mbiu ya Jumuiya ya Wazazi mwaka 2019"Elimu,malezi na maadili ni msingi wa uongozi Bora,chagua viongozi makini 2019" .
Robart alisema Zahanati ya MONGOLANDEGE inafaa kuwa kituo cha afya ina eneo kubwa maombi ya kupandishwa daraja wameyapokea watayafikisha Serikalini kwa utatuzi.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mongolandege Jimbo la Ukonga Hawa Lesso alisema kituo hicho kina kabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa gari la kubeba wagonjwa,ufinyu wa chumba cha kutunza dawa, uchakavu wa uzio unaozunguka zahanati hiyo,uchache wa Watumishi.
Aidha Hawa alisema huduma zinazotolewa ngazi ya zahanati lakini Jamii inayowazunguka ina uhitaji mkubwa wa huduma zaidi zitolewazo.
"Tunaomba mtusaidie kutatua changamoto tulizozianisha ukiwemo kupandishwa hadhi kituo chetu kutoka zahanati na kuwa kituo cha Afya kwani eneo lipo la kutosha "alisema Hawa.
Mwisho
Post A Comment: