Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma  kimewataka Wanasiasa wanaokichafua chama hicho ilikujipatia umaarufu kuacha mara moja tabia hiyo kwa kuwa wapo baadhi ya wanasiasa Wanawadanganya Wananchi kwa kukituhumu chama hicho  iliwaweze kuonewa huruma.

AKizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Dansani Shayo alisema kuna baadhi ya maneno yanasemwa na Wanasiasa akiwemo Mbunge wa Kigoma Mjini, kwamba Chama hicho kimewaaambia viongozi wa Serikali kwamba wasilete Maendeleo Kigoma kuwa suala hilo litampa ujiko Zitto Kabwe jambo ambalo sio la kweli.

Alisema Chama hicho hakijawahi kuzuia maendeleo kuletwa  Kigoma, kwa kuwa Chama hicho kinatekeleza ilani  ya CCM  na Serikali inayotekeleza miradi yote Kigoma na maeneo mengi  ni ya Chama hicho hivyo hawawezi kushindwa kutekeleza miradi au kuizuia Serikali kuleta maendeleo Kigoma kwa kuwa Watanzania wote ni wamoja.

Alisema Katika Mkutano wa Chama cha ACT wazalendo  kilichofanyika 1April mwaka huu  Kiongozi wa Chama Hicho na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe, alisema kwamba kamati ya Siasa ya Kigoma mjini ilipokaa na Waziri mkuu walimwambia  kwamba wasilete maendeleo katika jimbo hilo ikiwa  ni pamoja na kuboresha zao la mchikichi Kigoma jambo ambalo ni la uongo na la upotoshwaji wa wananchi.

Alisema kama Wanasiasa hao na Kiongozi huyo anataka kufanya Siasa, asifanye siasa za kusema uongo iliaweze kuonewa huruma isipo kuwa ajipange na kuongelea ni nini amefanya katika Kipindi ambacho alikuwa kiongozi wa jimbo hilo.

" mpaka sasa kuna miradi mingi imeletwa na Serikali ikiwemo mradi mkubwa Wa maji unaotekelezwa katika manispaa hiyo pamoja na barabara za manispaa ni fedha zilizo letwa na Serikali ya chama cha Mapinduzi  kwa ufadhili wa  Benki ya Dunia  na Kila siku Zitto anatembea  Nchi mbali mbali lakini mpaka sasa hakuna mradi wowote au aonyeshe wawekezaji aliowaleta kuleta maendeleo katika jimbo hilo", alisema Shayo.

Alisema Kwa sasa Chama hicho Kimejipanga  kuhakikisha Wanashinda  kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi taifa ,  kwa kuwa Wananchi wanaimani na Serikali iliyopo madarakani na  Viongozi wake wanajiamini kwa kazi wanayoyafanya na kazi zilizo fanywa  na  chama hicho.

Aidha Shayo alisema  kwa sasa Viongozi waliopo katika madaraka wa upinzani wajipage Kuondoka kwa kuwa kwa sasa Wananchi hawataki kudanganywa wanajiamini na wanajua nini Wanafanya.
Share To:

Post A Comment: