Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto
akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia
kuhusiana na usimamiza wa fedha zinazotolewa katika miradi mbali mbali
ya maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Homoud Jumaa
mara baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu zilizojengwa katika kituo cha
afya mlandizi pamoja na kujionea ukarabati wa chumba cha kuhifadhia
maiti

maiti.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
…………………………
VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais
Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo
amechukizwa kuona baadhi ya viongozi na watendaji kutotimiza majukumu
yao ipasavyo ikiwemo kufanya mambo kienyeji kwa kupokea miradi ya
maendeleo pasipo kufahamu mwenendo mzima wa mkataba ulivyo pamoja na
kutojua gharama za fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya utekelezaji.
Jafo ametoa kauli hiyo wakati
wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha afya cha mlandizi kilichopo
Wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kujieneo mwenendo mzima wa
ukarabati wa majengo pamoja na kujionea ujenzi wa majengo matatu ambayo
yamejengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 400 fedha ambazo zimetolewa na
serikali kuu.
Pia Jafo alibainisha kuwa hawezi
kuwavumilia watumishi ambao ni wazembe na wanashindwa kutimiza majukumu
yao ipasavyo na kuwataka kuachana mara moja na vitendo vya kujihusiha na
ubadhilifu wa fedha ambazo zinatolewa na serikali kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
“Mimi kama kiongozi wetu
sipendi kuona kabisa mnafanya kazi kienyeji bila ya kuzingatia sheria na
taratibu amabzo zimewekwa na nchi, na katika hili siwezi kulifumbia
macho maana maeneo mengine nimepita nimekuta miradi mingine bado inasua
sua nah ii ni baadhi ya watu kutotimiza majukumu yao ipasavyo ni
ninachotaka miradi yote inapokuja lazima wahusika kufahamu mikatab
ailivyo pamoja na fedha ambayo inatolewa sio kupokea tu,”alisema Jafo.
Aidha aliseama kwamba serikali
ya awamu ya tano kwa sasa imeshatoa fedha katika vituo vya afya zaidi
ya 90 hapa nchini kwa lengo la kuweza kuongeza majengo mengine pamoja
na kufanya ukarabati wa miundombinu ya wodi mbali mbali ikiwemo nyumba
za watumishi kwa lengo la kuweza kuboresha sekta ya afya kwa wananchi.
Aidha katika hatua nyingine
Jafo ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Kibaha vijijini kwa
kutekeleza agizo lake la kukukarabati chumba cha kuhifadhia maiti
katika kituo cha afya mlandizi ambapo hapo awali kilikuwa hakifanya kazi
kabisa kwani kiligeuzwa kuwa eneo la stoo na kuhifadhia vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Kibaha vijijini Butamo Nuru alisema kwamba
wametekeleza agizo ambalo walipatiwa na waziri wa Tamisemi la
kukarabati miundombinu ya chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na kununua
majokofu nane ambayo yamegharimi kiasi cha shilingi milioni 36.
WAZIRI Jafo katika ziara yake ya
kikazi kwa halmashauri ya Kibaha vijijini ameweza kukagua miradi mbali
mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa majengo matatu ya wodi ya
upasuaji,wazazi,na wagonjwa wa nje (OPD) sambamba na kutembelea miradi
mingine miwili ya ujenzi wa hospotali pamoja na jengo la ofisi za
halmashauri hiyo.
Post A Comment: