Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ofisi za wizara
zilizojengwa katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma
Machi 27.2019 (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandisi Valentino Chaffu,wakati alipo kagua jengo la Ofisi ya Rais (TAMISEMI) katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, katika mji
mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 kutoka kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.
Francis Michael,
katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Marry
Mwanjelwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
                     
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandisi Valentino Chaffu,wakati alipo kagua jengo la Ofisi ya Rais (TAMISEMI) katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandisi Valentino Chaffu,wakati alipo kagua jengo la Ofisi ya Rais (TAMISEMI) katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ofisi za wizara zilizojengwa katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) | 
WAZIRI
 MKUU Kassim Majaliwa amesema nia ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli ya
 kujenga upya mji wa Serikali imetekelezwa baada ya mji huo kukamilika 
kwa asilimia 99.
Ameyasema
 hayo leo (Jumatano, Machi 27,2019) alipotembelea mji mpya wa Serikali 
unaojengwa katika eneo la Mtumba, Jijini Dodoma. Majengo ya wizara 20 
yamekamilika.
Katika
 ziara yake hiyo, Waziri Mkuu ametembelea na kukagua majengo ya Wizara 
13, ambapo amesema ameridhishwa na hatua za ujenzi zilizofikiwa katika 
maeneo mengi.
Hata
 hivyo katika maengo hayo ya wizara 13 aliyoyatembelea, Waziri Mkuu, 
alibaini kasoro kwenye mlango wa kuingilia katika Ofisi ya Makamu wa 
Rais Muungano na Mazingira.
Kufuatia
 hali hiyo, Waziri Mkuu amemuagiza mkandarasi anayejenga jengo hilo 
auondoe na aweke mwingine kwa kuwa mbao zilizotumika zipo chini ya 
kiwango na haupendezi.
Kadhalika,
 kuhusu ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi 
ambayo bado haikamilika, Waziri Mkuu amemuongezea siku 10 mkandarasi na 
kumtaka akamilishe.
Wakati huo huo,
 Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri na Makatibu Wakuu wahakikishe kazi 
iliyosalia ambayo ni ya kuboresha mazingira ya nje ya ofisi hizo iwe 
imekamilika ifikapo Apriri 15, mwaka huu. Mji huo unatarajiwa 
kuzinduliwa na Rais Dkt. Magufuli.
Awali,
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira 
na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema ujenzi wa mji huo ulianza 
Desemba mwaka jana na ulitarajiwa ukamilike Februari mwaka huu lakini 
utakamilika Mei mwaka huu.
Waziri
 Jenista alisema ujenzi wa majengo ya wizara tatu ambayo hayajakamilika 
ikiwa ni pamoja na OR-TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Wenye 
Ulemavu yatakamilika Mei mwaka huu.
 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,             
41193 – Dodoma,
JUMATANO, MACHI 27, 2019.
Post A Comment: