Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga na chama hicho mwisho wa kufanya hivyo ni Disemba, 2018.
Polepole ametoa kauli hiyo jana Jumapili Oktoba 7, 2018 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ambapo amesema mwaka 2018 ndio mwisho wa chaguzi ndogo za ubunge, wale watakaoshindwa kuhamia CCM wabaki walipo.
“Tumezingatia na tunaweka jitihada zetu zote katika kushughulika na utatuzi wa shida za watu wetu wa Tanzania. Mwaka 2018 ndiyo mwisho kwetu kufanya chaguzi ndogo za ubunge kwa wale wanaohama vyama vyao na kujiunga na CCM. Watakaoikosa raundi hii mbaki hukohuko tutakutana 2020”, ameandika Polepole.
Jana kabla ya Polepole kutangaza maelekezo hayo mbunge wa Simanjiro (CHADEMA), James Ole Millya amejiuzulu nafasi zake zote ikiwamo ubunge na kujiunga na chama hicho(CCM)
Post A Comment: