Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara 'Bwege' anashikiliwa na polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai , Bwege alikamatwa jana saa 10 jioni eneo la Maalim Seif lililopo Kilwa Kivinje.

Ngubiagi amesema mbali na Bwege wengine wanaoshikiliwa na polisi ni madiwani wanne akiwemo diwani wa Kilwa Masoko na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: