Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema chama kikuu cha African National Congress kinatarajia kuanzisha mchakato bungeni wa kuimarisha marekebisho ya Katiba yaliyopendekezwa, kutengeneza njia kwa ajili ya kunyakua ardhi bila malipo iliyokuwa inamilikiwa na watu weupe.
Ramaphosa, ambaye ameahidi kurudisha ardhi hiyo kutoka kwa wakulima weupe tangu miaka ya 1600 hadi idadi ya watu mweusi kukosa ardhi.
Maphorisa aliongea hayo siku ya Jumanne kuwa “Imekuwa wazi kuwa watu wetu wanataka katiba kuwa wazi zaidi” juu ya pendekezo, ambalo linaonekana kuwa watu wachache wa Afrika Kusini weupe watolewe kwa nguvu kwenye mashamba”
“Ingawa Kumekuwa na hofu kutokea kwa uharibifu ambao utakuwapigo kwa kilimo cha biashara katika nchi yetu na inaweza kuiweka kwenye mgogoro wa uzalishaji wa chakula, kama ule ambao uliikumba Zimbabwe ambayo imetoka kupoteza usawa kwa wakulima weupe mwaka 1999-2000”
Rais huyo ataendeleza mpango wake wa kuimarisha ugawaji wa ardhi mwezi Machi, pia alitaka kuwahakikishia wananchi weupe, ambao hujumuisha asilimia 9 ya jumla ya idadi ya watu, kwamba serikali itashughulikia suala la utata kupitia “majadiliano, kwa ushirikino tutapata ufumbuzi mzuri ambao utapeleka nchi yetu mbele”
Post A Comment: