Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo, Ado Shaibu amefunguka kuwa hakuna mwanaharakati anayeweza kulitetea Taifa akiwa chini ya Chama tawala.

Shaibu amefunguka hayo katika mkutano wa wake na wanahabari jan, katika ofisi za Chama hicho ambapo alisema kuwa endapo wabunge, Nape, Bashe na Hawa Ghasia wana nia ya dhati ya kuwatetea wanyonge wahamie ACT-Wazalendo.

“Wabunge wanaotetea haki za wanyonge, wakina Nape, Bashe na Hawa Ghasia haiwezekani kufanya harakati za kuwatetea wanyonge huku mkiwa CCM, sana sana mtaonekana waasi katika chama chenu njooni kwetu”, alisema Shaibu.

Hayo yamejiri ikiwa ni siku chache kabla ya kuahirishwa kwa vikao vya Bunge, liliibuka sakata la korosho lililokuwa likiendelea katika vikao vya Bunge, ambapo Wabunge wa CCM ambao waliokuwa wakilipigia kelele suala hilo ni Hussein Bashe, Nape Nnauye pamoja na Hawa Ghasia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: