Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameutaka uongozi wa klabu ya Yanga kutoa jibu linaloeleweka hadi kabla ya Jumapili juu ya kujitoa kwao kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, (CECAFA KAGAME CUP).

Kauli hiyo ya Karia imekuja kufuatia Yanga kuiandikia barua TFF kuwaarifu kutoshiriki michuano hiyo kutokana na kubanwa na ratiba ya mashindano mengine.

Karia amesema kwamba amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na kutoridhishwa na sababu walizozitoa Yanga kwani hata timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo zina ratiba ngumu pia.

“Kabla hata hatujalipeleka suala hili CECAFA, nauomba uongozi wa Yanga hadi kufika jumapili uwe umetoa jibu la kueleweka juu ya mashindano hayo,”amesema Karia.

Aidha karia ameongeza kuwa kweney CECAFA KAGAME CUP kuna timu za Gor Mahia na Simba ambazo pia bado ziko kwenye michuano ya SportsPesa Super Cup hivyo kama kulalamikia ratiba zenyewe zingekuwa za kwanza kufanya hivyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: