Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ameziagiza
familia za askari waliouawa wakilinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) kumaliza haraka taratibu za mirathi.
Pia,
amesema Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo
amekwisha kuunda Baraza la Uchunguzi, kuchunguza kupotea kwa askari
mmoja aliyekuwa akilinda amani DRC.
Waziri Mwinyi ameyasema hayo jana Mei 14 wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19 ya Sh1.9 trilioni.
Waziri Mwinyi alisema tayari baadhi ya familia za askari hao zimeshakamilisha taratibu za mirathi.
Alisema fedha za mirathi zimetolewa kwa baadhi ya familia lakini zipo baadhi hazijakamilisha taratibu.
“Familia ambazo hazijakamilisha taratibu za mirathi zikamilishe haraka,” alisema.
Kuhusu
askari mmoja aliyepotea siku hiyo ya mapigano Waziri Mwinyi alisema:
“Umoja wa Mataifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,
wanaendelea kumtafuta na ikitimia miezi sita kwa Serikali ya Tanzania
tutaitisha uchunguzi na Mkuu wa Majeshi ameitisha baraza la uchungizi,”
alisema.
Alisema
baada ya hapo Mkuu wa Majeshi atatoa taarifa ya kifo. “Lakini huyu
kijana amepotea na mpaka sasa anatafutwa, hatuwezi kusema amepotea au
yuko hai.” Alisema
Post A Comment: